dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 9, 2016

Maalim Seif aeleza kilichomsibu

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Siku moja baada ya kuugua ghala na kulazwa kwenye chumba cha uangalizi maalumu (ICU), katika Hospitali ya Hindu Mandal,  Dar es Salaam, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema uchovu wa safari ni chanzo cha afya yake kuzorota.
 
Maalim Seif, ambaye jana aliruhusiwa kutoka hospitali, amesema  alikuwa anasumbuliwa na uchovu wa safari, baada ya kutoka India, alikokuwa amekwenda kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo jana, Maalimu Seif alisema hali yake iko imara, baada ya kupatiwa vipimo hospitalini hapo.
 
“Niko fiti kama mnavyoniona, Ninaweza kutembea kutoka hapa hadi Kibaha,” alisema Maalim Seif.
 
Alisema wiki iliyopita alikuwa nchini India kwa ajili ya matibabu na alirejea nchini Ijumaa na kwenda moja kwa moja  Zanzibar.“Jana (juzi) wakati nikija jijini hapa kwa ajili ya ratiba zangu za vikao kwa jioni, nilianza kujisikia kizunguzungu tangu nikiwa airport (uwanja wa ndege). Nililazimika kupanda ndege hivyo hivyo, nilipofika Dar es Salaam, nililetwa moja kwa moja hadi hapa hospitalini,” alisema Maalim Seif.
 
Alisema kwa sasa anaendelea vizuri na kwamba alikuwa akitarajia kuruhusiwa kwenda nyumbani jana jioni.
 
“Ninawashukuru wananchi, Wazazibari na Watanzania wote na wale walioko nje ya nchi wameonyesha mapenzi makubwa kwangu. Kweli wananchi wana mahaba na mimi, kwani wapo waliosikia nimelazwa na kuanza kuzimia, naomba niwajulishe ninaendelea vizuri na leo nitaruhusiwa,” alisema.
 
Kwa upande wake, Daktari wa Maalim Seif, Omary Suleiman, alisema walikwenda  India na kwamba Maalim Seif alifanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo na kurejea salama nchini.
 
“Tulirudi Ijumaa tukaenda Zanzibar na wakati anarudi Dar es Salaam jana kwa ajili ya shughuli za ratiba ya kikazi jioni alishikwa na kizunguzungu lakini haikutuzuia kusafiri kwa sababu ya majukumu yake ya kikazi kwani alikuwa na vikao,” alisema.
 
Alisema uchunguzi uliofanywa na madaktari hakuna ugonjwa wa aina yoyote unaomsumbua bali ni uchovu na kwamba hali yake inandelea nzuri.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment