Meli kubwa ya kitalii MS Hamburg imetia nanga bandari ya Zanzibar leo asubuhi ikiwa na watalii zaidi ya 400. Ilitarajiwa kuondoka jioni ya leo na kuendelea na safari yake.
Watalii hawa walishuka melini na kufanya safari za matembezi katika sehemu tofauti za kihistoria za mji wa Zanzibar na vitongoji vyake.
MS Hamburg ni meli ya kisasa ya kitalii inayomilikiwa na Conti Group na husimamiwa safari zake na Plantours Kreuzfahrten pamoja na na Ocean Tours ikiwa ni sehemu kampuni ya Akorn group (a division of Abercrombie & Kent).
No comments :
Post a Comment