zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 6, 2016

Muasisi wa ASP na Mwana Mapinduzi,Mhe. Mzee Hamid Ameir Amefariki Dunia Jana.


Mwana Mapinduzi na Mwanasiasa Mkongwe na Mwazilishi wa Chama ASP na CCM Zanzibar Mhe. Hamid Ameir amefariki dunia jana nyumbani kwake Mtoni Zanzibar.
Na taratibu za mazishi zinafanyika leo Kijiji kwao Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Maziko hayo yanafanyika asubuhi hii katika Kijiji cha Donge.
Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema Popeni 
Amin.

Maziko ya Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakibeba jeneza la Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kuswaliwa leo wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja
Wananchi waliohudhuria katika mazishi ya Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM wakilibeba jeneza wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na wananchi na Viongozi wakiwa katika maziko ya  Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM aliyezikwa  leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitia udongo katika kaburi la  Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kufariki jana katika hospitali ya Mnazi Mmoja na kuzikwa  leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakiitikia dua iliyoombwa  baada ya kuzikwa Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM  leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed akisoma risala ya wasifu wa Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kuzikwa leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]

No comments :

Post a Comment