Watu saba wanaosadikiwa kuwa majambazi walifanya uporaji huo baada ya kuvamia ofisi za kampuni ya simu za mikononi ya Halotel katika eneo la Medelii, Manispaa ya Dodoma, na kuwajeruhi askari polisi waliokuwa zamu.
“Ni aibu kumuona askari Polisi mwenye silaha ananyang’anywa silaha, ni aibu, na nasema hiyo ni aibu... mpaka jambazi akunyang’anye silaha na wewe una silaha?” Alihoji Rais Magufuli.
Rais Magufuli alizungumzia udhaifu huo siku tano zilizopita alipokuwa akihakiki bunduki zake mbili, shortgun na bastola, ikiwa ni utekelezaji wa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa wakazi wote.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa hapa, David Mnyambuga, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana, saa nane na nusu usiku katika ofisi hizo.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa hapa, David Mnyambuga, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana, saa nane na nusu usiku katika ofisi hizo.
Alisema watu hao wakiwa na mapanga na nondo, walivamia ofisi hizo na kutoboa ukuta na kisha kuwajeruhi askari polisi kwa mapanga na kupora SMG hiyo.
Aidha, alisema katika tukio hilo baadhi ya askari walipatwa na majeraha madogo ambapo walitibiwa na kuruhusiwa lakini Shadrack aliyejeruhiwa kichwani alilazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuruhusiwa jana asubuhi baada ya afya yake kuimarika.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa alisema jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja ambaye anaendelea kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo, na kwamba msako mkali bado unafanyika ili wahusika wote waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment