
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 20, baada ya ule wa Oktoba 25 mwaka jana kufutwa.
Samia alisema hayo juzi alipokuwa akifungua semina ya uhusiano wa wabunge wa Afrika ya Mashariki.
Alisema Tanzania imekuwa kinara wa demokrasia kwa kufanya na kumaliza uchaguzi wake kwa hali ya amani na utulivu.
“Nawahakikishia Watanzania na nchi wanachama wa jumuiya yetu, Serikali itahakikisha uchaguzi wa marudio Zanzibar unafanyika na kumalizika kwa amani na utulivu kama ilivyokuwa uchaguzi ulliopita,” alisema.
Samia aliwataka wabunge wa Afrika Mashariki kujadili kwa kina na kuweka mikakati ya kuwa na sheria na taratibu bora, zitakazoziwezesha nchi wanachama kuwa na uchaguzi huru na haki.
Spika wa Bunge la EALA, Daniel Kidega alisema nia ya semina hiyo ni kuweka mifumo mizuri ili kuwezesha uchaguzi katika nchi hizo kuwa wa demokrasia, unaofuata utawala wa sheria na huru na haki.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alisema semina hiyo licha ya mambo mengine, itajadili umuhimu wa kuwa na uchaguzi huru kwa kuzingatia usalama na amani ili kuendeleza ustawi wa demokrasia.
No comments :
Post a Comment