zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 22, 2016

Shein ashinda kwa asilimia 91.4

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) jana ilimtangaza Dk. Ali Mohamed Shein kuwa mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika juzi.

Mwenyekiti wa Zec, Jecha salim Jecha alisema kuwa Dk. Shein kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliibuka mshindi kwa kupata kura 299,982  sawa na asilimia 91.4.
Jecha alisema kwamba aliyeshika nafasi ya pili ni Hamad Rashid Mohamed (ADC) aliyepata kura 9,734 sawa na asilimia tatu.
Alisema sheria ya uchaguzi ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 42 inampa mamlaka ya kutangaza mshindi aliyepaya kura nyingi kushinda wenzake.
Vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo ni pamoja na ACT- Wazalendo, ADA Tadea,  ADC, AFP, CCM, CCK, Chauma,, CUF, Demokrasia Makini,  DP , Jahazi  Asilia,  SAU,  NRA na TLP.
Jecha ambaye amekuwa haonekani tangu alipotangaza kufuta uchaguzi wa Oktoba 2015 kwa madi ya kuwapo dosari nyingi, jana aliingia ukumbini akitokea chumba cha wageni mashuhuri (VIP).
Matokeo hayo yalitangazwa katika Hoteli ya Bwawani huku kukiwa na ulinzi wa Polisi, askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jecha alisema wapigakura walioandikishwa walikuwa 503,580, kura zilizopigwa ni 341, 865, zilizoharibika 13,538 na kura halali zilikuwa 328,357.
“Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kifungu cha 34 na sheria ya uchaguzi ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 429(4)  natamka na kumtangaza rasmi Dk. Ali Mohamed Shein wa Chama Cha Mapinduzi kuwa amechaguliwa kihalali na wananchi kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,” alisema. 
Wagombea wengine  na vyama vyao ni pamoja na Seif Sharif Hamad (CUF) ambaye alitangaza kutoshiriki uchaguzi huo. alipata kuta 6076 ingawa hakuwa na mawakala.
 Wengine ni na Juma Ali Khatibu (Ada Tadea) kura 1562 , Kasim Bakari Ali (Jahazi Asilia) kura 1470, Abdalh Kombo Khamisi  (DP), kura 512, Seif Ali Idd (NRA), kura 266, Issa Mohamed Zonga (SAU) kura 2018, Tabu Musa Juma, Demokrasia Makini kura 210 na Khamis Idd Lila (ACT- Wazalendo) kura 1225.
Wengine ni Said Soud Said (AFP) kura 1,303, Mohamed Masoud Rashi kura 493   na Hafidhi Hassan Suleiman (TLP) kura 1,496.
Tangu jana asubuhi kulikuwa na ulinzi mkali katika Hotel ya Bwawani na kila aliyeingia ndani ya ukumbi alikaguliwa na mashine maalum (Scanner).
Akizungumzia historia fupi ya mchakati wa uchaguzi huo, Jecha alisema Zec iliamua kuweka majina ya wagombea wa CUF kwenye karatasi ya kupigia kura licha ya kutangaza kujitoa kwa sababu wao walishateuliwa na tume tangu Septemba 6, mwaka jana kama wagombea.
Alisema kama kulikuwa na barua yoyote ya kutaka kujitoa ilitakiwa ipelekwe Zec kabla ya siku ya uteuzi na kwamba hakuna mgombea aliyefanya hivyo, badala yake alisikia wakitangaza kujitoa kupitia vyombo vya habari.
SOURCE: NIPASHE

No comments :

Post a Comment