Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, March 7, 2016

Dkt. John Magufuli amuapisha Balozi Eng. John Kijazi

[​IMG]

[​IMG]

[​IMG]

[​IMG]

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Hafla ya kuapishwa Balozi Kijazi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu wakuu na Naibu Katibu Wakuu.

Balozi Kijazi ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini ndia, anachukua nafasiya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na Mwakilishi wa Shirika Ia Umoja wa Mataifa Ia kuhudumia wakimbizi hapa nchini (UNHCR) anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amemshukuru kwa kazi kubwa ya kuhudumia wakimbizi kwa kipindi chote alichokuwepo hapa nchini.

Kwa upande wake Bi. Joyce Mends-Co le amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na Tanzania kuzisaidia nchi zenye matatizo, hususani migogoro ya kisiasa ambayo husababisha watu wake kuwa wakimbizi.

Pia amepongeza kuteuliwa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kusaidia usuluhishi wa mgogoro wa Burundi ambao umesababisha idadi kubwa ya wakimbizi kukimbilia Tanzania.

Hata hivyo amesema idadi ya wa kimbizi wanao kimbilia Tanzania imepungua kutoka wakimbizi 3,000 waliokuwa wakiingia hapa nchini kwa wiki, wakati Mgogoro wa Burundi ulipoanza hadi kufikia wakimbizi takriban i 1,000 wanaingia hapa nchini kwa wiki hivi sasa.

Aidha, Bi. Joyce Mends-Cole amewas hukuru watanzania kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi cha miaka mitatu aliyofanya kazi hapa nchini, na ameahid i kuwa Balozi wa kuitangaza vyema Tanzania.

GersonMsigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es salaam

07 Machi, 2016.

No comments :

Post a Comment