Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akihutubia wananchi na wanafunzi katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam.
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.
Mwanafunzi Saidat Proches akishukuru mara baada ya makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
|
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akiongea na walimu na wananchi mara baada makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
|
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiteta jambo na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani , Goodluck Charles katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
|
Wanafunzi wa shule ya msingi kawawa wakishuhudia makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam.
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga
Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.
Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo katika kata ya Mabibo katika manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.
“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali
zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa
miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, "amesema Gutierrez.
Gutierrez amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada
kama huo wa madawati katika shule za msingi katika
mikoa ya Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro na
kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa
madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.
Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye alisema madawati hayo 500 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Dar es Salaam na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.
“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Dar es Salaam. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 500 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,” alisema Makonda.
|
No comments :
Post a Comment