Ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kupitia Tanzania hadi katika bandari ya Tanga , Lenye urefu wa zaidi ya kilomita elfu moja mia nne, unatariajiwa kuanza siku za karibuni na kugharimu kiasi cha dola za kimarekani bilioni nne.
Dar es Salaam. Ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga nchini utaanza rasmi Agosti, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk James Mataragio akizungumza jijini Dar es Salaam jana, alisema ujenzi wa bomba la kilomita 1,403 utaanza miezi minne ijayo baada ya nchi hizo kufikia makubaliano.
Dk Mataragio alisema kuwa ujenzi huo utaanza baada ya kukamilika kwa hatua mbalimbali.
Ujenzi huo utagharimu Dola 4 bilioni za Marekanna kupitia katika mikoa ya Kagera, Singida mpaka Tanga. “Tunatarajia mapipa 60,000 ya mafuta yatakuwa yakisafirishwa katika bomba hilo kila siku,” alisema.
Alisema lengo la mradi huo ni kusafirisha mapipa 200,000 kila siku mpaka bandari ya Tanga ambayo itakuwa kiungo cha usafirishaji kwenda mataifa mengine.
Pia, alisema mradi huo unatarajia kutoa ajira 15,000 katika maeneo utakapopita katika kipindi cha miaka mitatu mpaka minne utakapokamilika.
Akizungumzia sababu za mradi kupita katika maeneo hayo na sabani za kuchagua bandari ya Tanga alisema: “Tumeichagua mikoa hiyo kwa sababu haina wakazi wengi na miinuko na gharama za uwekezaji zitapungua.”
Tanzania na Uganda ilisaini hati ya makubaliano ya ujenzi huo Oktoba 12, mwaka jana. Mradi huo utagharamiwa na Serikali ya Uganda na washirika wake.
No comments :
Post a Comment