Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 24, 2016

ZANZIBAR: Dk. Shein kuapishwa leo akiwa na siri Serikali ya Umoja Kitaifa.

Image result for DR SHEIN

Wakati leo ikiwa ni siku ya mapumziko Zanzibar lengo likiwa ni kutoa fursa kwa wananchi kushuhudia sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk. Ali Mohammed Shein, imeelezwa kuwa kitendawili cha kuwapo Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), kinaweza kuteguliwa kwa kutumia kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
 
Juzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, wakati akizungumza na Nipashe mjini Unguja kuhusu masuala mbalimbali yaliyojiri katika uchaguzi wa marudio, alitangaza mapumziko hayo ikiwa ni pamoja na maandalizi ya sherehe za kumwapisha Rais Mteule.
 
Katika uchaguzi wa marudio uliofanyika mwishoni mwa wiki, Dk. Shein wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliibuka mshindi wa kiti cha Urais wa Zanzibar baada ya kupata kura 299,982 sawa na asilimia 91.4.Waziri Aboud alisema viongozi wakitaifa na baadhi ya mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini na wa vyama vya siasa, wamealikwa na wamethibitisha kushiriki katika sherehe hizo.
 
Alisema viongozi wa kitaifa watakaoshiriki ni Rais wa Dk. John Magufuli, Makamu wake, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
 
MUUNDO WA SUK
Kitendawili cha kuwapo Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi huo, imeelezwa sasa kinaweza kuteguliwa na kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
 
Aidha, kama Rais wa Zanzibar, Dk. Shein atatumia kifungu hicho, kuna uwezekano wa aliyekuwa mgombea urais kupitia ADC, Hamad Rashid Mohamed, kushika nafasi ya Umakamu wa Kwanza wa Rais.
 
Mwanasiasa huyo amekuwa akitajwa katika siasa za Zanzibar kwamba anaweza kupewa nafasi ya Umakamu wa Rais, huku wengine wakisema anaweza kumteua tena Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alitangaza kujitoa katika uchaguzi mkuu wa marudio.
 
Kwa mujibu wa kifungu cha  53: ''Rais anayo mamlaka ya kuanzisha au kufuta ofisi Zanzibar na kuteua wakuu wa ofisi na kuwapandisha cheo kwa muda wa utumishi, kufukuzwa na kushughulika na hatua za kinidhamu kwa watu walioteuliwa kushika dhamana za ofisi hizo.''
 
Sehemu ya pili ya Katiba ya Zanzibar ambayo inazungumzia nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na Makamu wa Pili, kifungu cha 39(1), kinasema kutakuwa na Makamu wawili wa Rais ambao watajulikana kama Makamu wa Kwanza wa Rais na Makamu wa Pili wa Rais.
 
Katika kifungu cha 39 (2), kinasema ndani ya siku saba mara baada ya kushika madaraka, Rais atateua Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais.
 
Kifungu hicho 39 (3) pia kinasema Makamu wa Kwanza wa Rais atatakiwa awe na sifa za kumwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama kilichoshika nafasi ya pili katika matokeo ya kura za uchaguzi mkuu.
 
Sifa ya kumuwezesha mtu kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ni pamoja na kuwa na umri wa kuanzia miaka 21, asiwe mtu aliyewahi kufungwa kwa kosa la jinai, awe na akili timamu na awe raia wa Tanzania.
 
Katiba hiyo inaendelea kufafanua kuwa iwapo chama kilichoshika nafasi ya pili kimepata chini ya asilimia 10 ya kura zote za uchaguzi wa Rais, hakitakuwa na sifa ya kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
 
Aidha, kinasema ikiwa Rais amepita bila kupingwa, basi nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kitapewa chama chochote cha upinzani kilichoshika nafasi kwa wingi wa viti vya majimbo katika Baraza la Wawakilishi.
 
Kwa mujibu wa maelezo hayo ya Katiba ya Zanzibar, vyama vyote vya upinzani vilivyoshiriki uchaguzi wa marudio havina sifa za kuteua jina la mtu anayetakiwa kuteuliwa na Rais kushika nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kuwa havikupata asilimia 10 ya kura wala kiti hata kimoja cha uwakilishi wa majimbo.
 
Ofisa mmoja kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema mambo mawili yanaweza kutokea katika uundwaji wa serikali ijayo ya Dk. Shein.
 
Ofisa huyo alisema kama Rais atatumia kifungu cha 53 ambacho kinampa  mamlaka ya kuanzisha ofisi ama kuifuta na kuteua wakuu wa ofisi, anaweza kuwaingiza wapinzani ndani ya serikali yake.
 
Alisema wapinzani hao wanaweza kutoka chama chochote kikiwamo cha CUF, lakini ikiwa atatumia kifungu cha 39, anaweza kuwaacha nje na kuunda serikali ya chama kimoja cha CCM.
 
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga, amesifu vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuimarisha ulinzi katika kipindi chote cha uchaguzi.
 
Alisema ulinzi huo utaendelea kuimarishwa hususan leo wakati Dk. Shein anaapishwa na hakuna tukio lolote la uvunjaji wa amani hadi sasa limeripotiwa.
 
SOURCE: NIPASHE

No comments :

Post a Comment