dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 7, 2016

Bajeti tegemizi kwa asilimia 37.5 Makusanyo yafikia Sh. trilioni 8.9

SERIKALI imefanikiwa kukusanya trilioni 8.99 katika kipindi cha Julai 2015 hadi Februari, mwaka huu, katika makusanyo ya ndani yakiwamo ya halmashauri mbalimbali nchini ambayo ni sawa na asilimia 97 ya makadirikio.

  • Katika makadirio yake, ilipanga kukusanya Sh. trilioni 9.3 kwa kipindi hicho.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, akiwasilisha mapendekezo ya kiwango na ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2016/17 kwenye mkutano wa wabunge wote, jijini Dar es Salaam jana, alisema mapato ya kodi yalikuwa ni Sh. bilioni 7.9 sawa na asilimia 99 ya lengo la kukusanya Sh. trilioni 8.01.
Mpango alisema mapato yasiyo ya kodi yalikuwa ni Sh. bilioni 786 sawa na asilimia 86 ya lengo la kukusanya Sh. bilioni 916.1.
Alisema mapato yaliyokusanywa na halmashauri yalikuwa Sh. bilioni 270 sawa na asilimia 78 ya makadirio ya Sh. bilioni 347.9.
MISAADA NA MIKOPO
Waziri Dk. Mpango alisema hadi kufikia Februari, mwaka huu, washirika wa maendeleo walitoa jumla ya Sh. trilioni 1.01 ambazo ni sawa na asilimia 62.5 ya malengo ya Sh. trilioni 1.6 kwa kipindi hicho.
Alisema kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 169.6 ni za mikopo ya kibajeti sawa na asilimia 37 ya malengo ya Sh. bilioni 455.2.
“Kiasi cha Sh. bilioni 197 na Sh. bilioni 651.3 kilitolewa katika kipindi hicho kwa ajili ya mifuko ya kisekta na misaada na mikopo nafuu ya miradi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 99 na 67 ya lengo la kipindi hicho,” alisema.
Aliongeza: “Kutofikiwa kwa malengo ya mikopo ya kibajeti kulitokana na baadhi ya washirika wa maendeleo kupunguza ahadi zao, kuweka masharti mapya na wengine kuamua kutotoa fedha walizoahidi kutokana na kubadilika kwa sera ndani ya nchi zao zilizohusiana na misaada kwa nchi zinazoendelea.”
Aidha, alisema serikali itaendelea kufanya majadiliano na washirika hao ili kupata njia bora ya kuondoa changamoto zilizopo na hatimaye kupunguza athari za kibajeti.
Pia, alisema serikali itaendelea kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi wa kibajeti.
Alisema kutofikiwa kwa malengo ya upatikanaji wa fedha kwenye miradi ya maendeleo kunatokana na kasi ndogo ya utekelezaji wake na kuchelewa kutoa taarifa zake na kukwamisha kupata fedha nyingine.
MIKOPO YA NDANI
Mpango alisema hadi Februari, mwaka huu, serikali imekopa Sh. trilioni 3.7 ikiwa ni asilimia 101 ya kiasi kilichopangwa kukopwa.
Alisema kati ya kiasi hicho, Sh. trilioni 2.13 zilizokopwa kwa ajili ya kulipa amana za serikali zilizoiva na mikopo mipya, ilikuwa ni Sh. trilioni 1.6 sawa na asilimia 101.
“Serikali ilikopa zaidi katika soko la ndani kutokana na kutopatikana kwa wakati kwa mikopo ya nje, ukopaji huu haukuathiri viashiria vya uchumi ikiwa ni pamoja na viwango vya riba katika soko la fedha la ndani,” alifafanua.
MWENENDO WA MATUMIZI
Waziri wa Fedha alisema serikali imetoa mgao wa matumizi wenye thamani ya Sh. bilioni 13.5 kwenda kwenye mafungu mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti sawa na asilimia 92 ya makadirio ya bajeti hadi Febrauri, mwaka huu.
Alisema kati yake, Sh. trilioni 10.6 zilikuwa ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikijumuisha mishahara na malipo ya Deni la Taifa.
Mpango alisema mgawo uliotolewa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ni Sh. trilioni 2.6 na kwamba asilimia 86.6 ni fedha za ndani.
“Serikali imefanya malipo yaliyovuka mwaka 2014/15 yenye jumla ya Sh. trilioni 1.5 na kufanya jumla ya matumizi hadi Februari mwaka huu kuwa Sh. trilioni 14.7 sawa na asilimia 103 ya lengo la kipindi hicho,” alisema.
Alisema mwenendo wa matumizi katika kipindi cha Julai, mwaka 2015 hadi Februari, mwaka huu, ulizingaria mahitaji ya fedha katika mafungu yaliyokuwa yanatekeleza shughuli za uchaguzi mku pamoja na maamuzi mbalimbali ya serikali kama vile elimu ya msingi bure na ulipaji wa madeni yaliyohakikiwa.

/IPPMEDIA

No comments :

Post a Comment