dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 14, 2016

BREAKING NEWS!

Image result for breaking news

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanesco Mhandisi William Mhando na wenzake walioshtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi baada ya kukosekana na hatia.


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando na mkewe Eva Mhando .

Mhando na wenzake walikuwa wanashitakiwa kwa makosa sita likiwemo la matumizi mabaya ya ofisi, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mhando alikuwa anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake. 


Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa niaba ya Hakimu mwenye kesi hiyo Kwei Lusema amesema  upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha juu ya matumizi mabaya ya ofisi kwani Mhando alikuwa haingii kwenye vikao vya maamuzi ya bodi ya Tanesco kwa hiyo alikuwa hana ushawishi wa moja kwa moja kushawishi kampuni  ya Santa Clara ambayo ni ya mke wake ipatiwe tenda

No comments :

Post a Comment