dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 9, 2016

Dkt Shein Atangaza Baraza La Mapinduzi

Rais Wa Zanzibar Dkt. Shein atangaza baraza la mapinduzi huku akipunguza idadi ya wizara hadi kufikia 13.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza jipya Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.

Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo la Mapinduzi kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13 zenye Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7 na taasisi za wizara alizozivunja amezihamishia ambapo  katika baadhi ya wizara za sasa.

Mawaziri hao watawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.

Baraza la Mawaziri Zanzibar hao ni;
1). Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
      Mhe. Issa Haji Ussi Gavu.

2). Wizara nchi Afisi ya Rais Katiba  Sheria Utumishi wa Umma na utawala bora – 
     Mhe. Haroun Ali Sleiman.

    Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Katiba .Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora 
      Mhe. Khamis Juma Maalim.  

3). Wizara ya nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ 
      Mhe. Haji Omari Kheir.

4). Wizara ya nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa  Rais 
      Mhe. Mohammed  Aboud. Mohammed


5). Waziri wa Fedha na Mipango 
      Mhe. Dk. Khalid Salum Mohd.

6). Wizara ya Afya
      Mhe Mahmoud Thabit Kombo.

Naibu Wizara ya Afya .
      Mhe.Harusi Said Suleiman.

7). Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
      Mhe.Riziki Pembe Juma 

Naibu Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali.
      Mhe, Mmanga Mjengo Mjawiri.

8). Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.
      Mhe. Balozi Amina Salum Ali.

9). Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na Usafirishaji
     Mhe Balozi Ali Karume 

Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi na Usafirishaji 
Mhe.Mohamed Ahmed Salum.

10). Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo 
         Mhe.Rashid Ali Juma 

Naibu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo.
          Mhe.Chumu Kombo Khamis.

11).Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi
        Mhe.Hamad Rashid Mohd 

Naibu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi.
   Mhe.Lulu Msham Juma.

12).Wizara ya  Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.
        Mhe.Mauldine Castiko.

13). Wizara ya Maji Ardhi Nishati na Mazingira.

Mhe Said Soud na Juma Ali Khatib wateuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Mapinduzi


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum:

i.            Mhe. Said Soud Said – Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

ii.          Mhe. Juma Ali Khatib – Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum.
 
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 9 Aprili 2016.
    
Waheshimiwa wote waliotajwa wanaombwa wafike Ikulu Mjini Zanzibar kesho Jumapili tarehe 10 Aprili 2016
saa 3 kamili za Asubuhi kwa ajili ya kuapishwa.



(Dkt. Abdulhamid Y. Mzee),
KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI
NA KATIBU MKUU KIONGOZI,
ZANZIBAR.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Azungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar Wakati wa Kutangaza Baraza Jipya la Mawaziri Wake.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali viliko Zanzibar wakati wa kutangaza Baraza lake Jipya la Mawaziri Ikulu leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali viliko Zanzibar wakati wa kutangaza Baraza lake Jipya la Mawaziri Ikulu leo.


Waandishi wa habari wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza nao katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo asubuhi.
Mwandishi wa habari wa ITV na Redio One Farouk Karim alipata fursa ya kuuliza swali kwa Rais wa Zanzibar wakati wa mkutano huo na waandishi uliofanyika Ikulu Zanzibar leo.
Mwandishi wa habari wa Kituo cha TV cha Chanel Ten Munir Zakari akiuliza swali katika mkutano huo na Rais wa Zanzibar Dk Shein Ikulu Zanzibar.
Mwandishi wa Kituo cha TV cha Star Tv Ndg Abdalla Pandu akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
Mwandishi wa Gazeti la Zanzibar Leo Ndg Hafsa Golo akiuliza swali kwa Rais wa Zanzibar wakati wa mkutano huo na waandishi wa kutangaza Baraza la Mawaziri Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijibu maswali ya baadhi ya waandishi waliopata fursa ya kuuliza. 
Waandishi wa habari wakiwa makini wakifuatilia maelezo ya Rais wa Zanzibar Dk Shein, wakati akizungumza na Waandishi Ikulu Zanzibar.
Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na waandishi katika kutangaza baraza jipya la Mawaziri Zanzibar Ikulu leo.asubuhi Zanzibar.
Waandishi wa Habari Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Waandishi wa Habari Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waandishi wa habari Zanzibar, baada ya mkutano wake na Waandishi Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Katibu Mkuu Kingozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee na Washauri wa Rais Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari baada ya mkutano wake na Waandishi Ikulu Zanzibar.                                                            

No comments :

Post a Comment