dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 6, 2016

Hatimaye Magufuli atoka nje ya nchi

Rais John Magufuli
By Peter Elias, Mwananchi 
Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo anakwenda Rwanda, ikiwa ndiyo ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo, Novemba 5, mwaka jana.
Rais Magufuli alisimamisha safari za nje kwa watumishi wa umma isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwake au Katibu Mkuu Kiongozi ili kuokoa fedha nyingi ambazo zinatumika katika safari hizo na kuzielekeza katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Tangu kuapishwa kwake, Rais Magufuli amefanya safari za ndani pekee katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na Geita.
Ziara hiyo ya siku mbili nchini Rwanda itaanza kwa uzinduzi wa kituo kimoja cha ukaguzi katika mpaka wa Rusumo unaounganisha nchi hizo kisha kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Kwa mujibu wa taarifa ya kituo cha habari cha KT Press cha Rwanda, siku ya pili Rais Magufuli ataungana na wananchi wengine wa Rwanda katika kumbukumbu ya maadhimisho ya 22 ya mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994.
Rais Magufuli ambaye ameambatana na mkewe Janeth, ataweka shada la maua kwenye makaburi hayo na kuwasha mwenge maalumu. Baadaye Rais ataungana na Wanyarwanda katika matembezi maalumu, kabla ya kwenda kwenye mkesha utakaofanyika kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kasiga alisema akiwa Rusumo, Dk Magufuli atafungua kituo cha biashara ya pamoja “one stop border post’.
Umuhimu wa ziara
Ziara hiyo inatarajiwa kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya mataifa haya.
Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu kwa uchumi wa Rwanda kwa sababu asilimia 70 ya mizigo inayotumia usafiri wa majini, inapitia Tanzania.  

No comments :

Post a Comment