dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 9, 2016

JovagoTanzania yaipongeza Zanzibar kwa kuimarisha utulivu katika kipindi cha Uchaguzi 2016

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Bw Andrea Guzzoni, Meneja Mkazi wa Jovago Tanzania alifafanua kuwa pamoja na kuwa Uchaguzi wa Rais Zanzibar ulifanyika mara mbili lakini bado wananchi wamekuwa watulivu kiasi cha kufanya shughuli za kitalii kutoharibikika kama ilivyotegemewa.

“Zanzibar ni mji wa Utalii, Kama kungekuwa na vurugu za aina yeyote hii ingeharibu shughuli za kiserikali na soko la mji huu kwa kiasi kikubwa”. Aliongezea.

Kwa Upande wake, Lilian Kisasa, Meneja Mawasiliano wa JovagoTanzania, aliongezea kwa kusema kuwa watalii wengi waliokuwa wanaingia Zanzibar na kubook hoteli ni watanzania wenyewe, ambapo idadi ndogo ya watalii kutoka nje ilipungua kwa 5% tu, Hata hivyo haikuweza kuathiri soko la utalii kwa kiwango kikubwa.Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) iliweza kutangaza marudio ya uchaguzi visiwani humo baada ya matokeo yaliyopita kufutwa, ambapo, Dr. Ali Mohamed Shein alitangazwa rasmi kuwa mshindi wa marudio ya uchaguzi wa urais Zanzibar.

Aidha serikali imeombwa kuhimiza hasa utalii wa ndani kwani bado Watanzani wamekuwa wako nyuma katika kutembelea hifadhi zao wenyewe ambapo ,hatua hii ikiimarika itaweza kuongeza pato la taifa kwa asilimia kubwa.

Kuhusu Jovago

Jovago.com, tovuti inayorahisisha huduma za ku book hoteli kupitia mitandaoni. Ofisi kuu hapa Africa zipo Lagos (Nigeria), Nairobi kenya, na Dakar (Senegal). Jovago.com imegunduliwa na kampuni ya Africa Internet Group (AIG) chini ya udhamini wa MTN, AXA na Millicom

Jovago.com ni tovuti No.1 Inayoongoza katika huduma za ku book hoteli kupitia mtandaoni pamoja na kutoa huduma nzuri na za haraka kwa ufanisi wa kiwango cha juu cha urahisi wa matumizi ya tovuti hiyo. Jovago.com inazaidi ya hoteli 25,000 hapa Africa na hoteli 200,000 za dunia nzima kwenye tovuti. 

No comments :

Post a Comment