dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 7, 2016

Lazima uvuje jasho jasho tu!


  • WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amewasilisha Kiwango na Ukomo wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2016/17, akisema itakuwa Sh. trilion 29.53.
Kati ya fedha hizo, mapato ya ndani ni Sh. trilioni 17.79 ambazo kati ya hizo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kukusanya Sh. trilioni 15.1 na mapato yasiyo ya kodi yakiwa Sh. trilioni 2.69.
Hata hivyo, bajeti hiyo kubwa katika historia ya Tanzania na yenye kuleta matumaini, inaelezwa na wachambuzi wa masuala ya uchumi na kodi kuwa, itawalazimu Watanzania kuvuja jasho jingi na kukamuliwa katika nyanja ya kodi ili kuongeza mapato ya serikali iweze kutekelezeka kwa ufanisi.
Wachambuzi hao wanaeleza kuwa, ili serikali iweze kufikia kiwango cha bajeti hiyo, inapaswa kufanya jitihada kubwa na kuja na ubunifu wa kubuni vyanzo vipya vya mapato, hali ambayo kwa kiasi kikubwa itabebwa na wananchi ambao watalazimika kulipa kodi nyingi na baadhi ya bidhaa kuongezewa kodi ili kuziba nakisi ya wastani wa Sh. trilioni 2 itakayokuwapo kutokana na mamlaka hiyo kwa sasa kukusanya wastani wa Sh. trilioni 1.1 kwa mwezi.
Kiwango hicho cha makusanyo ya mwezi ambacho kwa uhai wa bajeti hiyo wa mwaka mmoja wenye miezi 12, hakiwezi kufikisha Sh. trilioni 29.53 zinazopangwa kutumika katika kipindi chote cha mwaka mzima, hivyo kuhitaji jitihada za ziada katika ukusanyaji mapato.
WAHISANI WAONGEZA UGUMU
Marekani imeshatangaza kuifuta Tanzania kwenye nchi wanachama wa Shirika la Changamoto za Milennia (MCC) ,hivyo nchi kukosa Sh. trilioni 1.03 ilizokuwa ipewe na mfuko huo kusaidia ujenzi wa barabara za pembezoni na kusambaza umeme vijijini.
Umoja wa Ulaya EU na ipo kwenye hatihati ya kutoa Sh. trilioni 1.56, ukiendelea kusubiri hatma ya mazungumzo na hali ya Zanzibar.
Pia baadhi ya mawaziri wa Uingereza nao wanaishauri serikali ya nchi yao kuifutia Tanzania msaada wa Sh. bilioni 622, kutokana hali ya Zanzibar.
Wizara ya Fedha na Uchumi pia imeshatangaza wahisani 10 kati 14 wanaosaidia bajeti kuu ya serikali kujitoa, ambapo Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Servacius Likwelile, alisema waliobaki ni Benki ya Dunia (WB), Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Dernmark na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB).
Hatua hiyo ya wahisani ni pigo kubwa kwa bajeti ya serikali ya mwaka huu, kwani mchango wao katika bajeti hiyo utakuwa umepungua.
Hata hivyo, Rais Magufuli inaonekana ameliona hilo na mara kadhaa amekuwa akiisisitiza TRA kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato, kubana mianya ya ukwepaji kodi na kukuwajibisha wanaotumia vibaya fedha za umma ili nchi iweze kujitegemea kimapato.
Aidha, Dk. Mpango alinukuliwa na vyombo vya habari akisema walishaona dalili ya wahisadi kutotoa fedha na kwamba serikali imeandaa bajeti bila ya kutegemea fedha hizo.
Wahisani wengine ambao wamekuwa wakisaidia bajeti kuu ya serikali ni Uingereza, Canada, Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Norway na Sweden.
Itakumbukwa kuwa, kwenye bajeti ya serikali ya 2014/15 wahisani walitarajiwa kuchangia Sh. trilioni 1.09, lakini wengi walikataa kutoa fedha kutokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.
MCHANGANUO WA BAJETI
Dk. Mpango akisoma hotuba yake mbele ya wabunge wote jijini Dar es Salaam jana, alisema makusanyo yasiyo ya kodi yanatarajiwa kuwa Sh. trilioni 2.69, huku makusanyo ya halmashauri zote yakiwa Sh. bilioni 665.41.
Alisema serikali inatarajia kupata Sh. trilioni 3.6, ikiwa ni misaada ya wahisani kwenye bajeti kuu ya serikali na miradi mbalimbali wanayoifadhili moja kwa moja.
Kwa upande wa mikopo ya masharti ya kibiashara, Dk Mpango alisema serikali inatarajia kukopa Sh. trilioni 2.1 kutoka vyanzo vya nje na Sh. trilioni 5.37 kutoka vyanzo vya ndani.
DENI LA TAIFA
Dk. Mpango alisema mpaka kufikia Februari, mwaka huu, deni la taifa lilikuwa ni dola za Marekani bilioni 19.93 ambazo ni sawa na Sh. trilioni 43.5.
AKIBA FEDHA ZA KIGENI
Kwa upande wa akiba ya fedha za kigeni, alisema mpaka sasa ni dola za Marekani bilioni 4.09 ambazo ni sawa na Sh. trilioni 8.936, kiasi ambacho kin awe za kununua vitu kutoka nje ya nchi kwa miezi minne.
Kwa upande wa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani, alisema imeendelea kupungua kutoka Januari 2015, ambapo dola moja ilikuwa Sh. 1,754.7 mpaka Februari, 2016 ambapo imekuwa Sh. 2,189.1.
MATUMAINI
Hata hivyo, pamoja na hali hiyo, bajeti hiyo ambayo imejikita kwenye kuendeleza viwanda vya kati na vikubwa, licha ya kuleta hofu ya kuwabana zaidi wananchi, inaweza kuwa faraja kwao kwani kwa mara ya kwanza fedha za maendeleo zitakuwa asilimia 40 ya bajeti yote.
Bajeti hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kwa serikali ya Rais Magufuli, inazidi ile ya mwisho ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, iliyokuwa ya Sh. trilioni 22.5, ambayo hata hivyo utekelezaji wake ulikuwa hafifu kutokana na kiasi kikubwa cha fedha za maendeleo kutowasilishwa licha ya kuwa umebaki mwezi mmoja kukamilika kwa mwaka wa fedha wa 2015/15. Mbali na bajeti hiyo ya mwisho ya Rais Kikwete ambayo ilijikita zaidi kufanikisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, bajeti ya mwaka 2014/15 ilikuwa Sh. trilioni 19.85 na ya mwaka 2013/14 ilikuwa Sh. trilioni 18.2.

/IPPMEDIA

No comments :

Post a Comment