dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 2, 2016

Mahitaji ya umeme nchini sasa yakamilika



Mradi wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi I umekamilika na kuingiza megawati 150 kwenye gridi ya Taifa, hivyo kufanywa megawati zinazohitajika nchini kwa sasa kukamilika.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uwekezaji Tanesco, Decklain Mhaiki alisema umeme sasa unapatikana wa kutosha, kwani megawati hizo zinawezesha kupatikana kwa megawati 1,500 ambayo ndiyo mahitaji kwa nchi nzima.

Alisema kwenye kituo hicho kuna mitambo minne ambayo tayari imefunguliwa kuruhusu gesi asilia kutoka Mtwara kuiingiza kwenye mitambo ya Tanesco, kwa ajili ya uzalishaji wa umeme katika kituo hicho cha Kinyerezi I.

Mhaiki alisema mradi huu umeunganisha maeneo yanayozalisha gesi asilia ambayo ni Mnazi Bay - Mtwara, Songo Songo, Kiliwani, Mkuranga na Ntorya. Alisema gesi iliyogunduliwa katika eneo la kina kirefu cha Baharí ya Hindi, mitambo yake miwili ilianza kufanya kazi tangu Oktoba mwaka jana na ikizalisha megawati 70.

“Hata hivyo kukamilika kwa uzalishaji wa megawati hizo, haimaanishi kwamba ndiyo matatizo ya kukatika kwa baadhi ya maeneo kutakuwa kumekwisha, kwa sababu hali hiyo inatokana na uchakavu wa miundombinu katika baadhi ya maeneo na Tanesco tunajitahidi kuiboresha sasa,” alisema.

Alisema changamoto nyingine ni hujuma ambazo zinafanywa na baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu, na watu wengine kwa kuiba mafuta kwenye transfoma.

“Ukweli ni kwamba wapo watumishi wasio waaminifu ambao wanahujumu huduma zetu kwa kuiba vifaa, nasi hatuna huruma nao tukiwabaini tunawafukuza kazi na kuwashtaki ili sheria zaidi ichukue mkondo wake,” alisema Mhaiki.

Awali, Wizara ya Nishati na Madini iliahidi kuwa kituo hicho kitajengewa uwezo wa kuzalisha megawati 335, ambapo mdhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) atafanya tathmini ya gharama ili kuona kama kutakuwa na unafuu wa bei za umeme nchini.

Wakati huohuo, Tanesco imeingia mikataba ya kuuza nishati hiyo kwa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Hilo lilibainishwa jana wakati wa mkutano wa 40 wa Shirikisho la Umeme kwa nchi za SADC (SAPP), unaoendelea jijini hapa na Tanesco kubainisha miradi miwili ya kusambaza umeme kwa nchi jirani.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhaiki alisema baada ya muda mrefu wa kutokuwa mwanachama hai wa SAPP, shirika hilo limejiandaa kutoa mchango unaostahili muda mfupi ujao. “Tumekutana ili kutafuta mbinu za kukabiliana na uhaba wa umeme uliopo ambao ni muhimu kwa maendeleo ya nchi zetu. Ili kuongeza mchango wetu, tunao mradi kutoka Iringa mpaka Shinyanga kupitia Dodoma ambao utazalisha 400 kv na mwingine kama huo utakaotoka Iringa mpaka Kabwe, Zambia kupitia Mbeya,” alisema Mhaiki.

Alifafanua kuwa mradi wa kwanza ambao unatarajiwa kutekelezwa kuanzia Septemba kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) utafanikisha usambazaji wa nishati hiyo jijini Nairobi, Kenya kupitia Arusha. Alieleza kuwa zaidi ya Sh700 bilioni zimeshapatikana na utakamilika mwaka 2018.

Kwa ule wa Iringa-Mbeya-Kabwe alisema upembuzi yakinifu kwa upande wa Tanzania umekamilika na Zambia inaendelea na unatarajiwa kufadhiliwa na Benki ya Dunia(WB), ili wananchi waanze kunufaika ifikapo mwaka 2019.

Mwenyekiti wa SAPP, Josh Chifumba alisema Tanzania itakuwa na mchango mkubwa kwenye uzalishaji wa umeme, hasa kutokana na rasilimali gesi iliyogundulika endapo miundombinu itakamilika kwa wakati. “Kila nchi inajitahidi kutumia rasilimali zake kuzalisha nishati ya kutosha kukidhi mahitaji. Kwa muda mrefu Tanzania haikuwa inanunua wala kuuza umeme kutoka kwa wanachama wenzake, lakini hatua zilizochukuliwa sasa, naamini zitaleta mabadiliko makubwa, alisema.

No comments :

Post a Comment