dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 9, 2016

NYARAKA ZA PANAMA: Dude linalotikisa vigogo duniani



By Julius Mathias, Mwananchi; jmathias@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Gumzo kubwa duniani kwa sasa ni kuhusu Nyaraka za Panama (Panama Papers) zilizofichua kashfa ya ukwepaji kodi na utakatishaji fedha kulikofanywa na viongozi wa mataifa mbalimbali, watu maarufu na wanasiasa.
Nyaraka hizo ni matokeo ya kazi iliyofanywa na kampuni ya Mossack Fonseca yenye makao yake Panama City, Panama ikijishughulisha na utoaji huduma za sheria hasa za kodi kwa taasisi na kampuni za kimataifa. Shughuli zake kubwa ni kuratibu matumizi sahihi ya misamaha ya kodi inayotolewa na mataifa tofauti duniani.
Kulingana na mabadiliko ya kiuchumi, matumizi ya misamaha ya kodi ni suala la kisheria na mataifa mengi yamekuwa yakitumia kigezo hicho kama moja ya mikakati ya kuvutia wawekezaji.
Nchini Tanzania, misamaha ya kodi imewahi kutolewa kwenye sekta ya uchimbaji madini, mawasiliano na hata kilimo kupitia mpango wa Kilimo Kwanza ambapo watu wenye uwezo waliruhusiwa kuagiza zana za kilimo kutoka kokote bila kulipia ushuru wa forodha kwa lengo la kuongeza tija kwenye sekta hiyo.
Nchi nyingine pia huwa na vipaumbele vyao ambavyo hutaka kuvikamilisha katika muda fulani na hufanywa kisheria. Mossack Fonseca imekuwa ikitoa huduma zake kwa kampuni za kimataifa zinazowekeza duniani kwa kigezo cha kupewa msamaha wa kodi.
Mfano, wafanyabiashara wa Urusi na Ukraine inaelezwa huwekeza zaidi nje ya mataifa yao ili kujikinga wasishambuliwe na wahuni pamoja na kupata faida kubwa zaidi duniani. Kwa hiyo, kupitia misamaha ya kodi kampuni na viongozi wa serikali wameitumia kujinufaisha.
Sheria za kodi hutaka kila mtu au kampuni kulipa kodi kutokana na kipato inachopata kulingana na shughuli zake za kila siku; iwe ndani au nje ya nchi. Kwa kuwa sheria za kodi za nchi nyingi ni kali, baadhi ya viongozi, wanasiasa na wafanyabiashara huamua kufungua akaunti katika nchi ambako ama hupata nafuu au hukwepa kodi au wanatakatisha fedha kutoka katika nchi zao.
Kwa mujibu wa nyaraka za Panama njia mbalimbali zinatumiwa na matajiri kukwepa kodi baadhi zikiwa kupitia uwekezaji wa kimataifa na misamaha katika nchi za ughaibuni ambako sheria si kali.
Walionaswa
Nyaraka za Panama zimefichua watu maarufu 143 duniani wakiwamo wakuu wa nchi 12 walioko madarakani na waliostaafu pamoja na familia zao na marafiki wa karibu ambao wamenufaika na ukwepaji kodi.
Miongoni mwao ni baba wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Davi Cameron, hayati Ian Cameron ambaye inadaiwa kila alipokuwa anakwenda kuhudhuria kikao cha bodi cha kampuni ya Blairmore Holdings, kwanza alikuwa anakwenda Uswisi au Bahamas. Awali David Cameroon alikana kuhusika katika kashfa hiyo lakini juzi alikiri kumiliki hisa katika kampuni ya baba yake ambayo iliuzwa kabla hajawa Waziri Mkuu.
Wabunge sita kutoka Bunge la Mabwenyenye (House of Lords), watatu wa chama cha Consevertive na wafadhili wa vyama vya siasa vya taifa hilo inaelezwa wana mali nje ya nchi ambazo hazilipiwi kodi.
Wengine ni Rais wa Russia, Vladimir Putin anadaiwa kuficha Dola za Marekani 2 bilioni (zaidi ya Sh4 trilioni) kwa kumtumia swahiba wake, Sergei Roldugin, ambaye ni mwanamuziki. Sehemu ya fedha hizo ambazo hutolewa kwenye benki za serikali ya Russia hufichwa kwenye hoteli ya Ski Resort ambako mwaka 2013 bintiye Putin, Katerina alifungia ndoa.
Nyaraka za Panama zimewataja pia shemeji yake Rais wa China, Xi Jinping; Rais wa Argentina, Mauricio Macri; na watoto watatu kati ya wanne wa Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif; Waziri mkuu wa mpito wa taifa hilo, Ayad Allawi pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Iraq. Pia, wamo mtoto wa Rais wa zamani wa Misri, Alaa Mubarak na Waziri Mkuu wa Iceland, Sigmundur Gunnlaugsson ambaye amejiuzulu.
Nyaraka hizo ndizo zimetumiwa kufichua kwamba Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino alisaini kandarasi na wafanyibiashara wawili ambao wanatuhumiwa kutoa hongo.
Vilevile, wamo Rais wa zamani wa Sudan, Ahmad Ali al-Mirghani; Naibu Jaji Mkuu wa Kenya, Kalpana Rawal; na mtoto wa aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, Kojo Annan. Inadaiwa watu hao walitumia kampuni hewa kununua nyumba katika mitaa ya kifahari jijini London, Uingereza ikiwa ni mbinu ya kutakatisha fedha.
Msaidizi wa karibu wa Mfalme wa Morocco, Mounir Majidi naye ametajwa kutumia kampuni kama hiyo kununua mashua ya kifahari mwaka 2006, lakini mawakili wake wanasema kuwa biashara hiyo ilikuwa halali.
Mpwa wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Khulubuse Zuma ametajwa kama mmiliki wa kampuni iliyotwaa hati ya kuchimba mafuta katika maeneo mengi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2010.
Zilivyopatikana
Taarifa hizi zilichapishwa Aprili 3 na gazeti la Ujerumani liitwalo Süddeutsche Zeitung kutoka katika chanzo chake cha siri na kuzitumia kwa pamoja na Umoja wa Waandishi wa Habari za Upelelezi (ICIJ) ambao ulizigawa kwa washirika wake wa kimataifa likiwemo gazeti la The Guardian la Uingereza na televisheni ya BBC.
Gazeti hilo lilisema lina nyaraka 11.5 milioni zilizokusanywa tangu miaka ya 1970 katika data zenye ukubwa wa terabaiti 2.6 sawa na GB2,600. Waandishi 370 kutoka vyombo vya habari zaidi ya 100 walitumia mwaka mzima kuzisoma, kuzielewa na kuzichambua taarifa hizo kabla hazijaachiwa na kuufikia ulimwengu mzima.
Kwa kuwa mafaili hayo ni mengi, kadri siku zinavyopita huenda wakatajwa Watanzania walioficha fedha ughaibuni kwa lengo la kukwepa kodi.

No comments :

Post a Comment