Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Friday, April 15, 2016

Polisi kukabidhi Bunge mkataba wa Lugumi leoKATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MEJA JENERALI PROJEST RWEGASIRA (KUSHOTO) AKIMSALIMIA KAIMU KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI, VICTORIA LEMBELI.
  • SIKU 10 za vigogo wa Jeshi la Polisi kurushiana mpira juu ya agizo la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu mkataba wenye harufu ya ufisadi wa Sh. bilioni 37 kati ya jeshi hilo na kampuni ya Lugumi Enterprises,...
Chombo hicho cha dola kimesema kitawasilisha mkataba huo ndani ya muda lililopewa leo.

Akizungumza na Nipashe jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, alisema mkataba huo utawasilishwa kwa wakati kama ambavyo Bunge limeagiza.

Kauli hiyo ya jana Meja Jenerali Rwegasira inakinzana na kauli zake ambazo amekuwa akizitoa tangu PAC itake kupewa mkataba huo.

Moja ya kauli yake kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu huyo alisema licha ya kwamba wizara ndiyo inayosaini mikataba iliyo chini ya taasisi zake, kwenye kupeleka mkataba huo haihusiki kwa sababu PAC iliagiza polisi iupeleke.
Kauli yake hiyo, ilitokana na ile ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Ernest Mangu, aliyetaka wizara iulizwe kwa madai kuwa wao ndio wanaohusika na mikataba mbalimbali ya taasisi zilizo chini yake.

“Sisi hatukuambiwa tupeleke mkataba huo kwenye kamati, kuna maelekezo maalumu tulipewa ambayo waandishi hamyajui,” alisema.

Lakini jana alibadili msimamo akisema: “Jeshi la Polisi lita-meet Deadline (litatoa kwa wakati) mkataba huo.”

TETESI ZA LUGUMI KUTOROKA
Kuhusu tetesi za Lugumi kutoroka kwenda nje ya nchi kama ni za ukweli, Meja Jenerali Rwegasira alisema kusafiri kwa mtu ni haki yake kwa sababu bado hajashtakiwa, hata hivyo hafahamu kama ametoroka kwenda nje ya nchi kama baadhi ya vyombo vya habari vinavyoripoti au la.

Alisema mahakama peke yake ndiyo yenye mamlaka ya kutoa zuio la mtu kusafiri na hufikia hatua hiyo endapo mtuhumiwa akifikishwa mahakamani.

Mojawapo ya watu wanaohusishwa kushiriki katika makubaliano ya mkataba huo ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Said Mwema, ambaye aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akieleza kuwa IGP ni ofisi, siyo mtu binafsi na jukumu hilo la -IGP alikwishalikabidhi kwa mtu mwingine ambaye ndiye anayetakiwa kulielezea.

Aprili 5, mwaka huu, PAC ilikutana na viongozi wa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kupitia mahesabu yao na kubaini kuwapo kwa mkataba huo tata ulioingiwa baina ya jeshi hilo na kampuni ya Lugumi wa ufungaji wa mashine za kuchukulia alama za vidole kwenye vituo vya polisi 108 wenye thamani ya Sh. bilioni 37.

Lakini inasemekana ni vituo 14 ndivyo vilivyofungwa mashine hizo, wakati kampuni hiyo ililipwa Sh. bilioni 34 sawa na asilimia 99 ya fedha zote, hali iliyoilazimu PAC kuhitaji kupatiwa mkataba huo ili kuupitia.

Hata hivyo, Aprili 11, mwaka huu, Jeshi la Polisi halikuwasilisha mkataba huo lilivyoagizwa, hali iliyowalazimisha wajumbe wa PAC kuliandikia barua na kulipa siku tatu hadi Aprili 15 (leo) liwe limewasilisha mkataba huo.

/Nipashe

No comments :

Post a Comment