dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 6, 2016

Salamu za Ponge za CCM kwa Dk Shein

SALAMU ZA PONGEZI ZA CCM

KWA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA
BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DKT. ALI MOHAMED SHEIN
KWA HOTUBA YAKE ALIYOITOA KATIKA UZINDUZI WA
BARAZA LA TISA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR
TAREHE 05 APRILI, 2016.

CHAMA Cha Mapinduzi Zanzibar kwa moyo mkunjufu kinampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kutokana na hotoba yake nzuri na dira kwa maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake, aliyoitoa jana Aprili 05, mwaka huu, wakati akizindua Baraza la Tisa (9) la Wawakilishi Zanzibar.

Ni hotuba iliyosheheni mambo kadhaa ya maendeleo kiuchumi, kisiasa na kiustawi wa jamii, mambo ambayo wananchi wanatarajia kuyaona yakitekelezwa na Viongizi wao wa Kitaifa kwa mustakbali wa Taifa na Wazanzibari wote.                                                                 

Chama Cha Mapinduzi, kimeelezea kufarajika kwake kutokana na hotuba ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Shein, alipoihakikishia jamii nzima ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla wake kwamba Serikali yake imekusudia kuwaleta maendeleo endelevu wananchi ndani ya maendeleo yao, na hivyo kuondokana na umasikini hasa wa kipato.Kupitia hotuba yake hiyo, wananchi walio wengi hasa wapenda amani, utulivu na maendeleo, wamejenga matumaini makubwa kutokana na kauli ya Mhe. Rais, na hasa pale alipowaahidi  kwa kusema Serikali yake iliopo madarakani na kupitia Mkuza II, itafanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na ustawi wa jamii, ili kuwawezesha Wazanzibari kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2020.

Akifafanua zaidi, Dkt. Ali Mohamed Shein, alisema huo miongoni mwa mikakati Serikali ya kuimarisha na kukuza uchumi wa nchi yetu na pia kukuza pato la Taifa. Ili kufika azma hiyo, kipaumbele cha mwanzo cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kukuza uzalishaji kupitia sekta za kilimo, utalii, viwanda vidogo vidogo, pamoja na kuimarisha raslimali watu, ubora wa huduma za jamii ikiwemo Elimu, Afya, Mazingira, Utawala bora, nk,  jambo ambalo linapaswa kupongezwa na kila mpenda maendeleo wa Taifa hili.

Akizungumzia kuhusu uimarishaji wa sekta ya biashara, Mhe. Dkt. Shein, amewataka Wazanzibari kutambua umuhimu wa zao la karafuu ambalo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar na kutoa wito kwa wananchi kuthamini juhudi zinazochukuliwa na Serikali yao za kuimarisha zao hilo, ili liweze kuwaletea tija zaidi.

Kama hiyo haitoshi,  kauli ya Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, ya kukubali kuwalipa wakulima wa karafuu kwa asilimia 80 ya bei ya zao hilo kwenye soko la dunia, inatoa matumaini mapya kwa wakulima wa zao hilo wa Unguja na Pemba.

Kuhusu suala la uwekezaji, Mhe. Dkt. Shein, amewaeleza Wazanzibari kuwa Serikali anayoiongoza imekusudia kushajiisha vyema wawezeshaji wa nje kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza hasa ujenzi wa hoteli za kisasa za kitalii na utoaji wake wa huduma ya fani hiyo, jambo ambalo kila Mzanzibari anatakiwa kuliunga mkono kwa nguvu zote.

Kauli ya Mhe. Rais wa Zanzibar  ya kuwahakikishia wananchi kutekeleza ahadi mbali mbali alizozitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ya kuimarisha maslahi ya wafanyakazi wa kima cha chini nchini kufikia Tsh. 300,000 kwa mwezi, pamoja na Idara Maalum za SMZ ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani, sio tu imeleta faraja kwa wananchi, bali pia itainua utekelezaji wa majukumu yao na kuleta tija kubwa kwa Taifa letu.

Sambamba na hilo, kauli ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanza kutekeleza kwa vitendo mpango wa kuwapatia pencheni maalum wazee wote waliofikia umri wa miaka 70 bila kujali historia ya kazi walizokuwa wakizifanya, nayo CCM linaunga mkono kwani zitawapunguzia kwa kiasi fulani ugumu wa maisha kwa wazee wetu hao pamoja na walio karibu na wazee hao. 

Kauli ya Rais wa Zanzibar kuendeleza na kuimarisha sekta ya michezo nchini, kwa kuimarisha mashindano mbali mbali Maskulini, Wilayani, Vikundi vya Mazoezi, pamoja na kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Mao Tse Tung, ni jambo jema kwa wananchi hasa wanamichezo wa Taifa hili.

Wazanzibari walio wengi wamefarajika kwa kiwango cha juu na kauli ya Rais wao mpendwa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa kuwaahidi tena bila ya kigugumizi kwamba wakati umefika kwa Serikali yake wa kutumbua majipu kwaviongozi na watendaji wote wanaoonekana kuwa ni majipu kwa maslahi ya Taifa na wananchi wake.

Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, kinachukua nafasi hii kumpongeza tena Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa uongozi wake mzuri ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tangu alipoingia madarakani (Awamu ya Kwanza) hapo Novemba 03, 2011.

Kwa mnasaba huo, katika Awamu ya Pili ya Uongozi wake, CCM inajenga matumaini makubwa yafuatayo :-

·        Mhe. Dkt. Shein, ataweza kuwaunganisha vyema Wazanzibari Ndani ya Serikali na Nje ya Serikali kwa kutekeleza kikamilifu Katiba na Sheria za nchi.
·        Mhe. Dkt. Shein, ataweza kusimamia kwa kiwango kikubwa na kuwaletea maendeleo ya haraka Wazanzibari jambo ambalo litawezesha kuimarisha ukuaji wa uchumi na huduma mbali mbali za jamii.
·        Mhe. Dkt. Shein, katika kipindi kijacho cha uongozi wake, ataweza kusimamia suala zima la amani na utulivu ndani ya visiwa vyetu vya Unguja na Pemba, jambo ambalo litawawezesha Wazanzibar wote kufanya shughuli zao za kisiasa, kiuchumi na kijamii, bila ya kuwa na hofu yoyote.
·        Mhe. Dkt. Shein, ni kiongozi anayependa watu wa rika na jinsia zote na hana chembe ya ubaguzi, anawapenda watu wote na atawatumikia wananchi kwa umakini na uadilifu mkubwa sana.

Mwisho, Chama Cha Mapinduzi kinatoa pongezi za pekee kwa Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuunda Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, itakayosimamia masuala ya maadili ya viongozi na nidhamu makazini.

Mwisho kabisa, Chama Cha Mapinduzi kinatoa wito kwa Jamii nzima ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla wake, wawe tayari kumpa kila aina ya mashirikiano, ili aweze kutekeleza kikamilifu majukumu yake aliyokabidhiwa na Taifa.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

(Vuai Ali Vuai),
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,
ZANZIBAR.
06/04/2016.

No comments :

Post a Comment