dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, April 10, 2016

Serikali yaendeleza subira Ziwa Nyasa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga aliyasema hayo wakati akizungumza na Nipashe kuhusu nini kinaendelea katika mgogoro huo.
Dk. Mahiga alisema serikali inasubiri taarifa itakayotolewa na kamati ya viongozi wa zamani wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wakiongozwa na Rais wa Zamani wa Msumbiji Joachim Chisano.
Alisema awali jopo hilo la marais wastaafu liliwahoji viongozi wa nchi zote mbili, kisha kukaa kikao cha peke yao na kutoa maamuzi.
"Tunasubiri waamue, jopo la wastaafu wakikaa na kuamua watatuambia," alisema Dk. Mahiga ambaye ni mwanadiplomasia wa mzoefu aliyepata kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa (UN).
"Kuna maswali walituuliza sisi na Malawi, lakini hatujui lini jopo hilo watakaa na kutupatia mrejesho.”
Mgogoro kuhusu ziwa hilo ambalo linajulikana kama Ziwa Malawi nchini Malawi na Ziwa Nyasa nchini Tanzania, ni wa muda mrefu.
Mgogoro huo uliongezeka baada ya Rais wa zamani wa Malawi, marehemu Bingu wa Mutharika, kuingia mkataba na kampuni ya Uingereza kutafiti uwezekano wa kuwapo mafuta ziwani humo.
Kwa sasa mgogoro huo unasuluhishwa na kamati ya viongozi wa zamani wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakiongozwa na Rais wa Zamani wa Msumbiji Joachim Chisano.
Ikitumia makubaliano ya kikoloni ya mwaka 1890, Malawi inadai kumiliki ziwa lote, ambalo inaaminika lina akiba ya gesi na mafuta, huku Tanzania ikisisitiza mpaka wake unaangukia katikati ya ziwa hilo.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliwahi kueleza kuwa Tanzania kamwe haitatumia nguvu kumaliza mvutano kati yake na Malawi kuhusu mpaka kati ya nchi hizo.Alisema Tanzania haioni mantiki ama busara ya kuingia vitani na nchi jirani kwa sababu yoyote ile.
Awali mgogoro huo ulishika kasi hali iliyolifanya Bunge la Tanzania kuingilia kati kupitia Kamati ya Mambo ya Nje chini kwa mwenyekiti wake wa wakati huo, Edward Lowassa ambapo lilitaka serikali kutumia diplomasia kumaliza.
Mbali na Chisano, wajumbe wengine wa jopo la marais wastaafu ni Festus Mogae wa Botswana na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, wanaosaidiwa na jopo la kimataifa la mabingwa wa sheria.

No comments :

Post a Comment