dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 4, 2016

Ukawa sasa Dar kuanza kutumbua majipu sugu Dar

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Charles Mwita

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, aliyetokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Charles Mwita, amesema mikatata tata iliyoingiwa na Jiji ukiwamo ule wa mabasi yaendayo kasi (Dart) na Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) pamoja na ule wa Kituo cha Mabasi Ubungo, itapitiwa upya na wanasheria kisha taarifa zake kuwekwa wazi kwa umma.
Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum mwishoni mwa wiki, Meya Mwita alisema: “Tutaita wanasheria na tutaipitia hadharani na tutawaeleza wananchi. Nina siku tatu ofisini, nipeni muda zaidi nitaeleza tuliyobaini kwenye mikataba husika.”
Meya huyo ambaye alichaguliwa na madiwani wa Chadema na wa CUF, alisema hakutakuwa na ubabaishaji katika mikataba hiyo kwani ndiko mapato mengi yanakopotea na kusababisha miradi ya maendeleo inayohudumia wananchi wengi kukwama ama kutotelekezwa.
“Ninachotaka bora mimi nife, lakini wananchi mpate haki, mmekuwa maskini kwa muda mrefu sana, mmedharauliwa vya kutosha, haiwezekani nchi ni yetu sote, siyo ‘majitu’ fulani yanakuja hapa yanatengeneza genge la wizi na kutajirika, wakati raslimali zipo na fedha za kutekeleza miradi ipo, kinachotakiwa ni usimamiaji na ufuatiliaji kuhakikisha hakuna shilingi inapotea,” alisisitiza na kuongeza.
“Tutaheshimiana hapa mjini Mungu ndiye ametupa Dar es Salaam, tutawatumikia sana kwa nguvu zote,” alisema Mwita ambaye ni diwani wa kata ya Vijibweni. 
Meya huyo alianza na mradi wa Uda kuwa atahitaji ripoti kutoka kwa waliokuwepo na kusoma kwa undani ndipo atakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia.
"Kituo cha Ubungo, mwaka jana kulikuwa na mpango wa kukihamisha kwenda Mbezi, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika, ninachosubiri ni ripoti ya kwanini waliamua kubomoa kabla hawajamaliza kujenga kituo mbadala," alisema na kuongeza.
“Tutaamua kwa pamoja katika kikao chetu cha Jiji kwamba tutaendelea na kituo kilichopo au Mbezi. Nina jambo la dharura nitakwenda kulifanya juu ya kituo hiki ambacho kinatoza fedha kwa watumiaji, lakini hakuna huduma za choo, kujikinga na jua na mpangiliop kwa ujumla,” alisema.
BODABODA
Meya huyo alisema hatakubaliana na kamatakamata ya waendesha pikipiki inayofanyika maeneo mbalimbali ya Jiji kwa kuwa vijana wanajitafutia riziki ya kuendesha familia zao.
“Hawa ni Watanzania wenzetu ambao serikali iliwanyima elimu, mtu akijiajiri tumuonee huruma, tumsaidie na siyo kumfanya awe maskini zaidi,” alisema.
Meya Mwita alisema suala la pikipiki kuingia katikati ya Jiji litajadiliwa kwenye vikao na kusikiliza walioamua kuwazua kwanini walifanya hivyo na kama inawezekana kuweka utaratibu wa muda wa kuingia na kutoka.
Alisema wengi wanakamatwa kwa makosa ya leseni, lakini kinachoonekana ni kukosekana kwa elimu, hivyo Polisi na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuwaelimisha umuhimu wa kuwa na leseni na bima za vyombo vyao.
“Nitaendelea kutoa elimu kwenye vyombo vya habari, nitawakusanya waendesha bodaboda wote nitaongea nao, pia madiwani wa vyama vyote tujadili kwa kina na kuwa na utaratibu maalum kwa ajili yao nao watoe elimu ya uraia kwenye kata zao,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment