dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, April 1, 2016

Zitto, Lissu wataka Magufuli ataje mshahara, akatwe kodi.


  Ikulu yasema wananchi wasubiri utekelezaji wa agizo la vigogo kukatwa mishahara waone ni nani ataguswa, Utumishi wasema utekelezaji umeanza
Siku tatu baada ya Rais John Magufuli, kueleza dhamira yake ya kupunguza mishahara ya watumishi wa umma aliosema wanalipwa mpaka Sh. milioni 40 kwa mwezi kwani hataki Tanzania kuwe na mtu analipwa zaidi ya Sh. milioni 15, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, wametaka kiongozi huyo wa nchi aweke mshahara wake hadharani na ukatwe kodi.

Mwaka 2013, Zitto alisema mshahara wa Rais ambaye kwa wakati huo alikuwa Jakaya Kikwete, ni zaidi ya Sh. milioni 30 na haukatwi kodi.

Kauli ya Magufuli

 Akizungumza mkoani Geita Machi 29, mwaka huu, Rais Magufuli alisema: “Nidhamu ya wafanyakazi waliokuwa wamejisahau, walifikiri hapa ni shamba la bibi, nina uhakika tumeanza vizuri, lakini hawajafika idadi ya tunaotaka kuwatumbua...wapo wafanyakazi katika nchi hii wanapata Sh. milioni 40 kwa mwezi na wapo wanaopata Sh. 300,000 kwa mwezi.

Nataka wale wa Sh. milioni 40, na hili nalisema kwa sababu mimi ndiye Rais, tutakata mishahara yao ishuke ili ikiwezekana, wataalam wangu wanafanyia kazi, pasije pakatokea Tanzania, asije akatokea Tanzania mtu anapata mshahara wa zaidi ya Sh. milioni 15.”
Zitto.

Zitto hakuishia hapo, pia alitaja mshahara wa Waziri Mkuu wa wakati huo, Mizengo Pinda, akidai kwamba kwa mwezi analipwa Sh. milioni 26, kati yake kukiwa na Sh. 11.2 za ubunge, Sh. milioni nane za uwaziri na Sh. milioni saba za Waziri Mkuu.

Jana, Zitto alisema azma ya Rais Magufuli ya kutaka kupunguza mishahara ya vigogo wa umma wanaolipwa mpaka Sh. milioni 40, ni njema, lakini ni busara kwanza akaweka wazi mshahara wake na akakubali ukatwe kodi kwa sababu kwa sasa haukatwi.

“Kila mara tumekuwa tukisema ni nini Rais analipwa na wao wanatoka wanasema taarifa tulizotoa siyo sahihi. Ni vyema sasa akaweka wazi mshahara wake na akakubali ukatwe kodi ili iwe mfano kwa watumishi wengine na hata Tanzania iwe mfano wa kuigwa na nchi nyingine,” alisema Zitto.

Lissu
Naye Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema ni vyema Rais Magufuli na wasaidizi wake wakaweka wazi mishahara yao na siyo ya watumishi wa mashirika pekee.

“Ni vizuri Rais akatuambia mshahara na marupurupu yake yote, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Manaibu, wasiishie kutaja mishahara ya mashirika pekee,” alisema.

Akitoa maoni kuhusiana na kauli ya Rais, alisema ili apunguze mishahara hiyo, lazima arekebishe sheria inayoruhusu Bodi za Mashirika ya Umma kujipangia viwango vya mishahara kulingana na wanavyozalisha.

Alisema hadi sasa hakuna sheria wala sera inayotaja kiwango halisi cha mshahara bali madaraja kwa watumishi wa Serikali Kuu na serikali za mitaa huku wa mashirika wakiachiwa huru baada ya serikali kuruhusu yajiendeshe kwa faida na kutoa nafasi ya kuwa na miakataba na watumishi na hivyo kuwa na uhuru wa kuamua mshahara.

“Watumishi wa mashirika hayo wanaajiriwa kwa mikataba maalumu ambayo hutaja nafasi anayopewa na kiwango cha mshahara, leo ukipunguza mshahara wake atakwenda mahakamani na kwa ushahidi wa mkataba atashinda kesi,” alisema.

 “Rais asifikiri anatawala Tanzania ya Nyerere, bali anatawala Tanzania ya miaka 30 baada ya Nyerere kuondoka. Hana mamlaka ya kupanga mishahara ya watumishi wa mashirika ya umma, kwa kuwa Bodi husika ndiyo zimepewa jukumu hilo. Asizungumze kufurahisha umma kwani atatengeneza vurugu kwenye mashirika husika,” alisisitiza.

Alisema watumishi wa mashirika husika huteuliwa na Rais kwa mujibu wa sheria na Bodi zimepewa mamlaka ya kisheria kupanga mishahara na marupurupu yao bila kuingiliwa, lakini kwa kuangalia uzalishaji uliopo.

Mathalani, alitolea mfano wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na maji (Ewura), analipwa mshahara mkubwa kuliko Katibu Mkuu wa Wizara ya Niashati na Madini kwa kuwa mmoja umepangwa na Bodi na mwingine kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma.

Aidha, Lissu alimshauri Rais kupanga viwango vya mishahara ambavyo vilifanyika wakati wa uchumi ambao ulisababisha watumishi wengi kuacha kazi kwenye mashirika ya umma na kwenda kwenye mashirika na kampuni binafsi.

“Mtu anasimamia shirika au mamlaka ambayo inajiendesha kibiashara na kuingiza mabilioni ya fedha, huwezi kumlipa sawa na mkurugenzi wa wizara ambaye anakaa ofisini kwa kazi za kawaida sana akisubiri fedha kutoka kwa mashirika,” alifafanua.

Lissu alisema kingine Rais anachoweza kufanya ni kuzielekeza Bodi zisipange misharara ya watumishi wa mashirika yao nje ya kiwango fulani, na kutoa tahadhari kuwa nchi itarudi miaka ya nyuma mashirika ya umma yalipangiwa mishahara na motisha wa kazi kushuka.

CWT
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania, Ezekiah Oluoch, akitoa maoni yake binafsi alisema ni lazima kuwe na timu ya kuchunguza kwa kina mishahara ya watumishi wa umma, sheria na kukutana na wawakilishi wa wafanyakazi na kujadiliana nao.

Kadhalika, watumishi wapewe nafasi ya kuamua iwapo kutakuwa na mabadiliko hayo waache kazi kwani wengine watahofia inaweza kushushwa na kuwaathiri katika pensheni zao, lakini kuwa na umakini na upunguzaji husika kwa kuwa yapo mashirika kama Benki Kuu Tanzania (BoT), ambayo viwango vyake ni vya kimataifa.

Aidha, alisema ni lazima serikali iliangalie suala hilo kwa kina kwa kuwa kuna mashirika yanayozalisha fedha nyingi inahitaji kuwapa motisha watumishi, huku akitolea mfano Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa haiwezekani watumishi wake walipwe sawa na wengine kwani ndiyo mwanzo wa kukaribisha rushwa.

TUCTA 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), Nicholaus Mgaya, alisema serikali inapaswa kuandaa sera ya mishahara ambayo itaeleza viwango vya kila mtu kulingana na nafasi na elimu yake.

Kuhusu kupunguza mishahara, alisema linawezekana kwa wale ambao wako kwenye mamlaka ya uteuzi wake, lakini kwa watumishi wengine wanalipwa kulingana na Sheria ya Utumishi na Mahusiano Kazini.

“Kupunguza mishahara kuna uzuri na ubaya wake. Mishahara minono wanayolipwa inatokana na makato tunapolipa umeme, maji na mafuta. Serikali iangalie kwa kina ili mishahara isipishane sana na kuzuia malalamiko,” alisema.

“Kumlipa mtu Sh. milioni 40, ni sawa na kusema anatumia Sh. milioni moja kila siku huku mwingine akipata mshahara duni kabisa,” alisema.
 
KATIBA
Hata hivyo, kama mshahara wa Rais utakuwa juu zaidi ya kiwango anachotaka, itakuwa ni vigumu kuupunguza kutoka na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Ibara ya 43-(1) ya Katiba hiyo inasema: “Rais atalipwa mshahara na malipo mengineyo na atakapostaafu, atapokea malipo ya uzeeni, kiinua mgongo au posho, kadiri itakavyoamuliwa na Bunge, na mshahara, malipo hayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo hicho, vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.”

Sehemu ya pili ya Ibara hiyo inasema: “Mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais, havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.”

KAULI YA IKULU
Akizungumzia hatima ya Rais kujipunguzia mshahara, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa, alisema: “Jambo la msingi tusubiri Rais atakavyotekeleza hiyo azma yake, ataitekeleza namna gani, kwa sababu hoja yake ilikuwa wapo watu wamejitengenezea utaratibu na wanajilipa mishahara mikubwa kupitia bodi zao.

“Kwa hiyo yeye anafikira kwamba katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi, wale wa chini ambao wana mishahara midogo sana, waboreshewe maslahi na wale wanaojilipa fedha nyingi, wana mishahara mikubwa ambayo yeye mwenyewe anasema Sh. milioni 40, serikali yake inafikiria kuweka wastani wa Sh. milioni 15.

“Tusubiri tuone wakati ukianza utekelezaji tuone imegusa watu gani, Rais anafanya haya kwa maslahi mapana ya wananchi, anatafuta namna ya kuboresha maisha ya watu wa chini, naamini utekelezaji ukianza, tutaona nani kaguswa na vigezo gani vimetumika.”

WAZIRI UTUMISHI
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala bora Angela Kairuki, alipoulizwa juu ya mshahara anaolipwa Rais na Waziri Mkuu, alisema haufahamu na hawezi kuzungumzia suala hilo.

Kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais watumishi wengine, Kairuki alisema watafanyia kazi agizo hilo na baada ya kuikamilisha watakabidhi ripoti kwa Rais ili utekelezaji uanze mara moja.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment