dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, July 16, 2016

MASAUNI ATOA ONYO KALI KWA ASKARI NA MAAFISA ZIMAMOTO MWANZA WATAKAOZEMBEA KATIKA KAZI, AKAGUA VITENDEA KAZI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Askari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Mwanza alipofanya ziara mkoani humo kwa lengo la kujua jinsi Jeshi hilo linavyofanyakazi mkoani humo. Masauni katika hotuba yake aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi na waepuke kutoa sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya uzimaji moto na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, ACF Hamidu Nguya akitoa maelezo ya utendaji kazi wa Jeshi lake mkoani humo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia). Masauni katika hotuba yake aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi na waepuke kutoa sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya uzimaji moto na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali. Kushoto ni Mratibu Msaidizi wa Jeshi hilo, Mussa Kaboni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akiangalia jinsi askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wanapokuwa wanazima moto katika matukio mbalimbali. Kulia ni Kaimu Kamishna wa Jeshi hilo Mkoa wa Mwanza, ACF Hamidu Nguya. Masauni alifanya ziara katika Ofisi za Jeshi hilo jijini Mwanza kwa lengo la kujua jinsi gani jeshi hilo linavyofanyakazi mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kuzungumza na Askari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Mwanza. Masauni aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi na waepuke kutoa sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya uzimaji moto na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwasalimia Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Mwanza wakati alipokuwa anawasili katika ofisi za Jeshi hilo, jijini Mwanza. Masauni aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi na waepuke kutoa sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya uzimaji moto na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti), Kaimu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, ACF Hamidu Nguya (wanne kulia) na akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi hilo mkoani humo. Masauni alifanya ziara katika ofisi za Jeshi hilo kwa lengo la kujua jinsi gani jeshi hilo linavyofanyakazi katika matukio mbalimbali jijini Mwanza. Hata hivyo, Masauni aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi na waepuke kutoa sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya uzimaji moto na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali

No comments :

Post a Comment