Na Himid Choko
Afisi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, inapenda kuwakumbusha wananchi kwamba, katika Mkutano wa Pili wa Baraza la Tisa la Wawakilishi la Zanzibar (Mkutano Uliopita) Miswada minne ilisomwa kwa mara ya Kwanza ambayo pia inatarajiwa kusomwa kwa mara ya Pili na mara ya Tatu pamoja na kujadiliwa katika Mkutano ujao utakaoanza tarehe 21/9/2016. Miswada yenyewe ni kama ifuatayo:-
1. MSWADA WA SHERIA YA (UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI) MAFUTA NA GESI ASILIA, 2016.
Mswada huu pamoja na mambo mengine utakuwa na lengo la kuanzisha Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPDC) ambayo itashiriki katika shughuli za utafutaji na uendelezaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
2. MSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA SUZA NA MAMBO MENGINE YANAYOHUSIANA NA HAYO.
2. MSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA SUZA NA MAMBO MENGINE YANAYOHUSIANA NA HAYO.
Mswada huu una lengo la kuunganisha Taasisi ya Uongozi wa Fedha (ZIFA), Taasisi ya Maendeleo ya Utalii (ZIToD) na Chuo cha Sayansi ya Afya (CHS) kuwa chini ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
3. MSWADA WA SHERIA YA KUANZISHA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR NA MAMBO MENGINE YANAYOHUSIANA NA HAYO.
3. MSWADA WA SHERIA YA KUANZISHA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR NA MAMBO MENGINE YANAYOHUSIANA NA HAYO.
Mswada huu unalenga kupendekeza kuanzishwa kwa Taasisi ya Elimu Zanzibar, ambayo itakuwa ni wakala wa Serikali na itakuwa na jukumu la kuandaa mitaala, vifaa vya kufundishia, kufanya tafiti za elimu zinazohusiana na maendeleo ya mitaala na kuimarisha vifaa vya kujifunzia ili kuhakikisha utoaji wa elimu kwa wananchi.
4. MSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALI MBALI NA MAMBO MENGINE YANAYOHUSIANA NA HAYO.
4. MSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALI MBALI NA MAMBO MENGINE YANAYOHUSIANA NA HAYO.
Mswada huu unarekebisha baadhi ya vifungu vya Sheria; zikiwemo Sheria ya Mahusiano Kazini, Sheria ya Mahkama za Mahakimu, Sheria ya Mahkama ya Biashara, Sheria ya Madawa na Usambazaji Haramu wa Madawa ya Kulevya, Sheria ya Mashirikiano baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria ya Biashara, Sheria ya Chuo Kikuu cha Kilimo Kizimbani na Sheria ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo. Marekebisho hayo yanayopendekezwa katika Sheria hizo ni kwa ajili ya kufanya marekebisho ya makosa yaliyomo katika Sheria hizo na vile vile kuweka masharti bora ili kwenda sambamba na malengo ya kuwepo kwa Sheria husika.
Nakala za miswada hiyo zinapatikana katika Afisi za Baraza la Wawakilishi zilizopo Chukwani kwa upande wa Unguja na Mtemani kwa upande wa Pemba au unaweza kutembelea katika tovuti ya Baraza la Wawakilishi www.zanziassembly.go.tz .
Wananchi wote mnakaribishwa kutoa maoni yenu kuhusu Miswada hiyo si zaidi ya tarehe 9, Septemba 2016. Maoni hayo yatapelekwa kwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kwa kufanyiwa kazi na mazingatio.

Maoni yatumwe kupitia anauni zifuatazo:-
1. Sanduku la Posta (S.L.P. 902, Zanzibar)
2. Barua pepe (zahore@zanlink.co au
3. Yaletwe Afisi ya Baraza iliyopo Chukwani
1. Afisi ndogo ya Baraza la Wawakilishi – Wete Pemba .
Ahsante,
Imetolewa na;
Afisi ya Baraza la Wawakilishi,
P. O. Box 902,
Zanzibar.
17 August 2016
No comments :
Post a Comment