Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) linakaribisha maombi ya kujaza nafasi tupu katika kada mbali mbali kwa waombaji wenye sifa stahili kwa ajili ya Unguja na Tawi la Pemba kama ifuatavyo:
UNGUJA
1. MHANDISI UMEME ( ELECTRICAL ENGINEER) - Nafasi 1
Sifa za muombaji
© Awe na shahada au stashahada ya juu ktk fani ya umeme (degree or advance diploma in Electrical Engineering or Electrical and Electronics Engineering )
© Umri usiozidi miaka 40 ifikapo mwezi wa septemba,2016.
© Ujuzi wa kutumia kompyuta ni sifa ya ziada.
2 FUNDI UMEME ( ELECTRICAL TECHNICIAN) -Nafasi 3
Sifa za muombaji
© Awe na stashahada ktk fani ya umeme (Ordinary diploma in Electrical Engineering).
© Umri usiozidi miaka 35 ifikapo mwezi wa septemba,2016.
© Awe na Ujuzi wa kutumia kompyuta.
3 FUNDI SANIFU (ARTISIAN) -
Nafasi 6
Sifa za muombaji
© Awe amehitimu na kupata cheti cha VETA.
© Awe amehitimu na kupata cheti cha elimu ya sekondari.
© Umri usiozidi miaka 30 ifikapo mwezi wa septemba,2016
4 DEREVA ( DRIVER ) -Nafasi 4
Sifa za muombaji
© Awe amehitimu na kupata cheti cha elimu ya sekondari
© Awe na leseni ya udereva
© Umri usiozidi miaka 35 ifikapo mwezi wa septemba,2016
- Nafasi 2
Sifa za muombaji
© Awe amehitimu na kupata cheti cha elimu ya sekondari
© Umri usiozidi miaka 35 ifikapo mwezi wa septemba,2016
© Aliepata mafunzo ya ulinzi atapewa kipao mbele.
PEMBA
1 DEREVA (Driver) - nafasi 3
Sifa za muombaji
© Awe amehitimu na kupata cheti cha elimu ya sekondari
© Awe na leseni ya udereva
© Umri usiozidi miaka 35 ifikapo mwezi wa septemba, 2016.
© Ujuzi wa ufundi gari ni sifa ya ziada.
2 MTUNZA GHALA ( STORE KEEPER ) - nafasi 1
Sifa za muombaji
© Awe amehitimu na kupata cheti cha manunuzi na ugavi ( certificate in procurement and supply management )
© Awe amehitimu na kupata cheti cha elimu ya kidato cha nne.
© awe na umri usiozidi miaka 30
JINSI YA KUTUMA MAOMBI.
Muombaji anatakiwa kuandika barua ya maombi na aambatanishe
@ Barua ya sheha wa shehia anayoishi muombaji
@ Vivuli (photocopy) vya vyeti vya kumalizia masomo , kitambulisho cha mzanzibari na leseni ya madereva.
@ maelezo binafsi (curriculum vitae ) ya muombaji.
@ Kila muombaji anatakiwa kuainisha juu ya bahasha nafasi anayoiomba .
Maombi yanaweza kutumwa kwa lugha ya kiswahili.
Mazingatio;
Muombaji anasisitizwa kuandika namba yake ya simu ktk barua yake ya maombi kwa mawasiliano.
Maombi yote lazima yatumwe kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo
MENEJA MKUU,
Shirika la Umeme,
S.L.P 235,
Zanzibar.
Au
Meneja Tawi,
Shirika la Umeme,
S.L.P 102,
Pemba.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 22/08/2016 .
AHSANTE.
No comments :
Post a Comment