Top Leaderboard Advert

Patreon

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 20, 2016

CCM ZANZIBAR YASHAURI MAALIM SEIF AZUILIWE HAFLA ZA KITAIFA!Maalim Seif Shariff Hamad

Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema ni wakati mwafaka sasa kwa Serikali kumzuia Maalim Seif Shariff Hamad ambaye alikuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kuhudhuria hafla za kitaifa.

Vuai amesema chama chake kimefadhaishwa na kuhuzunishwa na kitendo cha Maalim Seif ambaye aliwahi kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar kabla ya kurejeshwa kwa siasa za ushindani kushindwa kumpa mkono Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein walipokutana kwenye msiba wa Rais wa pili wa visiwa hivyo, Aboud Jumbe.

"Nawaomba watu wasiendeleze sakata hili kwasababu linamdhalilisha Maalim. Hatukutarajia kiongozi kama Maalim kufanya kitendo kama kile," amesema.

/Mwananchi.

1 comment :