Top Leaderboard Advert

Patreon

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 20, 2016

TANZIA: MSANII MKONGWE WA MUZIKI WA TAARAB, BI. SHAKILA SAID AFARIKI DUNIA!

Msanii mkongwe wa muziki wa Taarab, Bi. Shakila Said amefariki dunia usiku huu katika Hospitali ya Temeke jijini Dar.

Habari zilizotufikia muda huu kuwa Msanii mkongwe wa muziki wa Taarab nchini Bi. Shakila Saidi amefariki dunia usiku huu muda mfupi baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Shani ambaye ni mtoto wa mwisho wa marehemu ameithibitishia kuwa Bi Shakila hakuwa anaumwa ila baada ya kumaliza kuswali alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali alikokimbizwa alikutwa amekwishafariki.
Taarifa za kifo cha msanii huyo nyota mwenye umri wa miaka 70 zilianza kusambaa mitandaoni usiku, na kuhanikiza katika redio mbalimbali ambazo zilianza kucheza muziki wa mkongwe huyo ambaye wakati wa uhai wake alibahatika kuzaa watoto 15, 12 wakiwa hai.
Kwa mujibu wa taarifa za kifo cha mtunzi na mzimbaji huyo wa nyimbo wa kundi la JKT Taarab, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo ukisubiri taratibu za mazishi. Shakila alianza muziki mwaka 1961 akiwa na umri wa miaka 15.


Sikiliza moja ya nyimbo alizotamba nazo

Shakila Kifo Cha Mahaba Hakina Aibu
a

No comments :

Post a Comment