dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 6, 2016

CUF YATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI BAADA YA MAALIM SEIF KUREJEA ZANZIBAR KUTOKA UGHAIBUNI!

SALIM BIMANI - MKURUGENZI WA CUF WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO KWA UMMA

Katibu Mkuu wa The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi), Maalim Seif Sharif Hamad, amekamilisha hatua ya pili ya ziara zake katika nchi mbalimbali duniani na amewasili mjini Zanzibar, leo Ijumaa tarehe 5 Agosti 2016.

Maalim Seif Sharif Hamad, akiambatana na ujumbe wake maalum akiwemo Mkurugenzi wa mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa, alizitembelea nchi za Uingereza, Belgium, na kuhitimisha ziara yake hiyo nchini Netherlands katika mji wa Hague ilipo Mahakama ya kimataifa inayoshughulika na kesi zinazohusiana na makosa ya uhalifu dhidi ya Ubinadamu.

Aidha, Maalim Seif Sharif Hamad, alipata mualiko rasmi wa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama cha Democratic cha nchini Marekani uliolenga kumuidhinisha na kumpitisha mgombea Urais wa Marekani kupitia chama hicho, Bi. Hilary Clinton uliofanyika tarehe 28 Julai, 2016.

Sambamba na Mkutano Mkuu huo wa Chama cha Democratic Maalim Seif Sharif Hamad aliandaliwa mkutano wake maalum na kukutana na viongozi wa kiserikali, watunga sera, wataalamu na wanasiasa wenye ushawishi mkubwa katika nchi mbalimbali duniani, ambapo aliwasilisha mada ya Zanzibar na wajumbe kupata nafasi ya kujadili juu ya ulazima na uharaka wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kukabiliana na ukiukwaji wa demokrasia na uvunjifu wa Haki za binadamu kwa mustakbali wa wananchi na ustawi wa demokrasia nchini.Akizungumza na wananchi waliofika nyumbani kwake Chukwani Zanzibar baada ya kukamilika kwa Mapokezi yaliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Abubakar Khamis Bakar, Maalim Seif Sharif Hamad aliwataka wananchi kuendelea kuwa na uvumilivu na kusubiri matokeo ya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na wadau mbalimbali wanaofuatilia kwa kina kadhia ya yanayoendelea Zanzibar.

Kuhusu suala la kesi ya ukiukwaji wa Haki za Binadamu zinazoendelea kufanywa hapa nchini, Maalim Seif alisema kwamba CUF-Chama Cha Wananchi kinaendelea na mchakato wake wa kuwashitaki wahusika wa ukiukwaji na uvunjwaji wa Haki za Binadamu katika mahakama ya International Criminal Court (ICC) ambapo wakili wa kusimamia kesi hiyo amepatikana na kukabidhiwa jukumu la kusimamia kesi hiyo.

Ziara hiyo ya Maalim Seif Sharif Hamad ambayo ilimkutanisha na viongozi na watendaji wa serikali na wa taasisi za kikanda na kimataifa katika nchi alizozitembela, ikiwemo Umoja wa Ulaya (EU) ililenga kuelezea kwa kina hali mbaya ya demokrasia Zanzibar kufuatia kuvurugwa kwa makusudi kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 25 Oktoba, 2015 na kufutwa kwa matokeo yake yote.

Maalim Seif Sharif Hamad pia, alitumia fursa hiyo kuitanabahisha jumuiya ya kimataifa juu ya matendo kandamizi ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa, kwa mashirikiano baina ya makundi ya maharamia yaliyopo Zanzibar na vikosi vya Ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa lengo la kuwanyamazisha wananchi wanaodai haki yao ya kuheshimiwa kwa maamuzi ya kidemokrasia waliyoyafanya katika Uchaguzi wa Oktoba, 2015.

Kukamilika kwa ziara hii, ya awanu ya pili, ya Maalim Seif Sharif Hamad kunatoa fursa ya kuendelea kwa hatua nyengine za kutafutiwa ufumbuzi mgogoro wa kisiasa Zanzibar unaotokana na Uchaguzi Mkuu wa 25 Oktoba, 2015.

HAKI SAWA KWA WOTE

SALIM BIMANI
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO KWA UMMA

No comments :

Post a Comment