dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 16, 2016

Dk. Shein, Maalim Seif ‘bifu’ kali msibani!

Hali hiyo imedhihirisha namna chuki za kisiasa visiwani humo zilivyotamalaki ambapo Maalim Seif na Dk. Shein ndio mara ya kwanza kukutana uso kwa uso baada ya Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika tarehe 20 Machi mwaka huu visiwani Zanzibar.
Dk. Shein ndiye aliyekuwa akiongoza mazishi ya Alhaj Jumbe ambaye alikuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) aliyefariki Jumapili wiki iliyopita.
Kwenye msiba huo, baada ya Dk. Shein kusalimiana na wageni wengine kwa kuwapa mkono, alipofika kwa Maalim Seif, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), aligoma kupokea mkono wake.
Baada ya Maalim Seif kutopokea mkono wake, Dk. Shein aliunyoosha tena kwa matumaini kwamba kiongozi huyo wa CUF angeupokea, hata hivyo Maalim Seif aligoma.
Kutokana na mgomo huo, Dk. Shein alilazimika kumruka na kuendelea kusalimiana kwa kupeana mikono na viongozi wengine waliohudhuria maziko hayo.
Hatua hiyo imepokewa kwa hofu na baadhi ya waombolezaji waliokuwepo kwenye eneo hilo na walioshuhudia tukio hilo.
Hali hiyo inatafsirika kuwa ni kilele cha chuki za kisiasa zilizochochewa na Tume ya Uchaguzi visiwani Zanzibar (ZEC) chini ya mwenyekiti wake Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu kinyume na Katiba ya visiwa hivyo.
Kabla ya tukio hilo, visiwani Zanzibar kumeripotiwa kuwepo kwa ubaguzi wa kisiasa katika mambo mbalimbali ikiwemo huduma za kijamii ambapo wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanalalamika kutengwa na wale wa CUF.
Miongoni mwa maeneo yanayolalamikiwa kuwepo kwa ubaguzi huo ni katika uuzaji wa bidhaa dukani, usafiri wa daladala pamoja na vikao vya pamoja vya kijamii.
Mara kadhaa Jeshi la Polisi limekuwa likimwita Maalim Seif kwa mahojiano kutokana na matukio mbalimbali yanayoendelea visiwani humo.
Hata hivyo Jeshi la Polisi visiwani humo wamekuwa waoga kueleza kiini cha mahojiano hayo ambapo viongozi wa CUF wamekuwa wakieleza kuwa ni kutokana na tuhuma za uchochezi.
Serikali ya Dk. Shein inayumba kutokana na baadhi ya Wazanzibari kuipa mgongo kwa tuhuma kwamba, urais aliotunukiwa na NEC hauna ridhaa ya wananchi wa visiwa hivyo.

http://mwanahalisionline.com/dk-shein-maalim-seif-bifu-kali-msibani/

No comments :

Post a Comment