Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Friday, August 12, 2016

Hotuba ya Rais Magufuli Furahisha, Mwanza!

Streamed live on Aug 11, 2016 
Rais Magufuli: Ndugu zangu uchaguzi umekwisha hakuna aliyeshida wala aliyeshindwa bali Watanzania wote tumeshinda. 

Rais Magufuli: Niliahidi jiji la Mwanza litakuwa jiji la biashara tumeanza naomba mtuamini. 

Rais Magufuli: Watumishi walikuwa wanachukua ndege wanaenda Dubai wanafanya siku 3 au 4 wanarudi kwa gaharama za watoto wa masikini. 

Rais Magufuli: Mpaka sasa wafanyakazi hewa bado wapo na nitaendelea kutumbua. 

Rais Magufuli: Tumeanza kutoa fedha bil 18.77 tulizoziokoa kwenye hao mafisadi tukazipeleka kwenye elimu watoto wasome bure. 

Rais Magufuli: Wale Wabunge watiifu ambao hawakuziba midomo na kutoka nje, walipitisha tril. 29.5 za bajeti. 

Rais Magufuli: Katika fedha hizo tunataka tununue ndege 3 kubwa, air Tanzania ilikuwa na kandege kamoja. 

Rais Magufuli: Fedha ambazo tumetenga kwenye bajeti hii hazijawahi kutengwa toka dunia iumbwe. 

Rais Magufuli: Tanzania tulikuwa tumezoea masherehe kweli, wakubwa serikalini wakiona kuna sherehe wanajipanga kula. 

Rais Magufuli: Nimeambiwa kandarasi anatakiwa akabidhi hii kazi mwezi wa 12, unanisikia, nikisema nimesema. 

Rais Magufuli: Wewe kandarasi ukichelewesha mradi, tena ninyi Wahehe mkichukia mnajinyonga, basi utajinyongea hapo hapo darajani. 

Rais Magufuli: Upanuzi wa barabara ya Airport usiishie Pasiansi muongeze mpaka Airport na mimi hela nitawaletea. 

Rais Magufuli: Tunataka tuanze kutengeneza nguo kisha tuvae, alafu mitumba tuwapelekee Ulaya. 

Rais Magufuli: Wakakataa kuingia Bungeni, wakaziba midomo na plastiki, walisahau wangeziba na masikio, wakatoka na Bungeni. 

Rais Magufuli: Hakuna ulazima wa mtu unavua samaki mpaka vifaranga, mlinichagua nami nitawaambia ukwe. 

Rais Magufuili: kama kuna mtu alichoma makokoro ni mimi, na samaki waliongezeka. 

Rais Magufuli: Wanapita kuna polisi, uhamiaji, TRA, lazima tulinde rasilimali yetu ili watanzania waweze kufaidika. 

Rais Magufuli: Hizo zana zinapitishwa kwenye mipaka, shikeni na hilo gari mtaifishe moja kwa moja kwa sababu hayapiti angani. 

Rais Magufuli: Waziri wa Ushirika, ni heri ukose kula, mimi nitakuchagua kwenye viti maalum, lakini mali za Nyaza zirudi. 

Rais Magufuli: Nitoe agizo, ni lazima pawe na maeneo mbali mbali, muweze kufanya biashara, ila mkubaliane.

No comments :

Post a Comment