dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, August 10, 2016

WALEVI SASA KUKIONA ZANZIBAR!

  • Ulevi kutinga baraza la wawakilishi kutungiwa sheria Zanzibar!

TUME ya kurekebisha Sheria Zanzibar imeifanyia marekebisho sheria ya vileo ambayo ilikuwa na malalamiko mengi.

Akizungumza na Nipashe visiwani hapa, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Bakari Mshibe, alisema sheria hiyo ni ya muda mrefu kabla ya mwaka 1964 na Wazanzibari wengi hawaitaki kwa madai kuwa hawataki ulevi utungiwe sheria.

Hata hivyo, alisema Sera ya Serikali haijakataza kutumia ulevi kwa wale wenye kutumia haswa ikizingatiwa kuwa jamii imegawanyika licha ya dini zote kukataza ulevi.

Alisema lengo la sheria hiyo ni kutengeneza adabu katika matumizi ya ulevi ili mwenye kutumia ulevi atumie kwa nidhamu bila ya kuwaudhi watu wengine.

Alisema marekebisho yaliyofanywa yameweka adhabu ikiwamo kutokuwepo na baa karibu na makazi ya watu, nyumba za ibada, maeneo ya shule na ni marufuku baa kuuza ulevi muda wa asubuhi na mchana.

“Lengo siyo kukataza ulevi, lakini mwenye kutumia ulevi atumie kwa adabu ambazo serikali inataka, ndio maana vifungu vingi katika sheria hiyo ni makatazo ya watumiaji wa ulevi ikiwamo ulevi kutouzwa nyakati za mchana,” alisema Mshibe.

Alisema baada ya kuona matatizo ya ulevi yanayotendeka Zanzibar ndipo serikali ikaamua kurekebisha sheria ya vileo na kuweka misingi mema ya utumiaji wa ulevi kwa watumiaji.

“Matumizi ya ulevi yalikuwa ni holela ulevi ulikuwa ukiuzwa katika maduka ya kawaida ya vyakula huo ni utovu wa adabu, mtu alikuwa akinunua bia akitembea nayo hadharani huku anakunywa…sheria hii itadhibiti hali hiyo,” alisema.

Aidha, alisema marekebisho yasheria hiyo yanatarajiwa kuwasilishwa katika kikao kijacho cha Baraza la Wawakilishi.

Alifafanua kuwa itakapopitishwa, hata magari yatakayokuwa yamebeba vilevi yatafunikwa turubali bila ya wananchi kujua magari hayo yamebeba kitu gani.

Alisema utaratibu utakaotumika kusafirisha pombe kutoka bandarini utakuwa ni wa usiri mkubwa kama utaratibu unaotumika wakati vyombo vya ulinzi vinaposafirisha silaha akieleza kuwa huwa zinasafirishwa kutoka bandarini kwa muda maalumu usiku au alfajiri na huwa zinafunikwa ili kutowatia hofu wananchi hivyo na ulevi utasafirishwa kwa utaratibu huo.


/NIPASHE

No comments :

Post a Comment