dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 3, 2016

Hotuba ya Rais Magufuli kisiwani Pemba, Zanzibar!

Magufuli: Uchaguzi umeshakwisha na utakuja tena 2020, huo ndio ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Uchaguzi umekwisha mimi nikachaguliwa kuwa Rais na naitwa John Pome Magufuli na nimefunga Makufuli yote na funguo nimeshatupa. 

Nataka niseme Mhe Dk Shein, wewe ndie Rais na inawezekana umekuwa mpole kidogo, huo upole weka pembeni, unasapoti yangu yote, atakaekuchezea chezea niambie hata kwa kuninong'oneza. 

Tushirikiane kwa nguvu zote, wanaojaribu kuchezea amani yetu, mimi niliwahi kwenda Libya, mojawapo ya nchi za Afrika zilizokuwa na raha ni mojawapo. Pakajitokeza watu wachache kwa kuahidiwa ahadi za uongo, Libya leo siyo mahali panapokalika, watu wanamwaga damu kila siku, watu walichezea amani, hata amani inalevya. 

Rwanda wakati wa genocide walikufa watu wanaokaribia milioni moja, mmenichagua kuwa Rais wenu, nna wajibu wa kuwaeleza ukweli, wanaofanya chokochoko tunawajua wengine, wafatilieni wote wanaochomachoma washughulikiwe wote bila huruma.
Mna bahati mna Rais mpole sana na hata sura yake nzuri tu na ni Rais alietoka Pemba, ni kitu gani kinatusumbua. 

Mimi nilifanya nae kazi nikiwa naibu waziri na waziri, ninamfajhamu Dk Shein, mpeni ushirikiano. Kuna mtu alijifungia kwenye chumba alafu akasema ametoka Ulaya, msikubali kudanganywa, hivi karibuni alinunua Meli na zinafanya kazi, kuna maeneo mengi yamepelekwa maji na umeme, watu hamtaki kuyaona haya. 

Palikuwa na Prof Mbarawa hapa mkamkataa jimbo la mkoani(Mkanyageni) mkamkanyagia hukohuko, mimi nnafahamu umuhimu wake na nikachukua wizara tatu nikaziunganisha zote nikampa mtu aliekanyagwa huku. Mpeni ushirikiano Dk Shein, imebaki miaka minne tu na kitu na kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hiki ndio kipindi chake cha mwisho. Nawaomba wananchi tujenge umoja wetu. 

Tukienda kwa umoja wetu tutafanikiwa, tunataka tuimarishe uvuvi, mazao na serikali iliongeza hela kununua karafuu japo pato lake limeanza kushuka, tunataka tujenge hii nchi. Katika kipindi kifupi Pemba itakuwa kama Ulaya na wanaoharibu Pemba ni watu wachache sana. 

Wengine wanasema uchaguzi utarudiwa, kwa kawaida ndoto huwa ni usiku lakini hizo ni ndoto za usiku, lakini ukimkuta mtu anaota mchana, huyo anatafuta ukichaa. 

Nampongeza sana nh Jecha kwa kusimamia uchaguzi na umeenda vizruri sana na kama kuna tuzo mheshimiwa Shein utatoa, Jecha umpe hizo tuzo. Napongeza sana vyombo vya ulinzi, mmefanya kazi nzuri sana, mmesimamia amani ya Tanzania kwa uzalendo mkubwa sana.

No comments :

Post a Comment