dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 4, 2016

RAIS MAGUFULI AAHIDI KULINDA MUUNGANO NA KUDUMISHA AMANI!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa atasimamia kwa nguvu zote masuala yote yanayohusu maendeleo, kudumisha Muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar na kudumisha amani kwa faida ya wananchi.

Rais Magufuli amesema hayo jana tarehe 03 Septemba, 2016 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Zanzibar katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kibandamaiti Mjini Unguja.

Dkt. Magufuli ambaye aliongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli alisema ili mambo hayo yafanikiwe Wananchi wa Zanzibar hawana budi kukataa kujihusisha na vitendo vya vurugu na kuvunja amani na amewaonya watu wanaochochea vitendo hivyo kuacha mara moja.


Aliwataka wananchi wa Zanzibar kujihadhari dhidi ya wanasiasa ambao wanapandikiza chuki, ubaguzi na fitina, kwani watu hao wanataka kubomoa misingi mizuri ya umoja, upendo na mshikamano wa Taifa uliojengwa na waasisi wa Taifa hili.Rais Magufuli alimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein aliyehudhuria mkutano huo, kwa hatua mbalimbali anazozichukua kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar huku akibainisha kuwa tatizo la maji linalovikabili visiwa vya Zanzibar litakwisha baada ya kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa maji utakaofadhiliwa na Serikali ya India kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 92, na mradi mwingine utakaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 21.

Aidha, Rais Magufuli alivipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri vinayofanya katika kusimamia amani visiwani humo huku akivihakikishia kuwa yeye akiwa kiongozi wao anawaunga mkono.

Pamoja na Rais Shein Mkutano huo ulihudhuriwa na Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume, Mawaziri na Viongozi wa Siasa na Dini.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Unguja

No comments :

Post a Comment