dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, September 29, 2016

Samuel Sitta apelekwa Ujerumani kwa ajili ya matibabu!

  • Pia, ona hapa chini sababu alizozitoa Mhe Samuel Sitta juu ya uraia pacha!


Mwanawe, Benjamin Sitta amesema: “Anachoumwa ni miguu. Baba yupo katika hali nzuri, yupo salama tu, achaneni na taarifa za mitandao.” Alikuwa akirejea taarifa zilizoenea kwenye mitandao kwamba baba yake yu mahututi.
Septemba 19, Rais John Magufuli alimtembelea Sitta nyumbani kwake ambako alimueleza kuwa hali yake inaendelea vizuri. Taarifa ya Ikulu ilieleza mwanasiasa huyo mkongwe alikuwa jijini kwa ajili ya matibabu bila kueleza ugonjwa unaomsumbua.

Siku moja baada ya Rais kumtembelea, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa naye alikwenda kumjulia hali. Vivyo hivyo, Septemba 21 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alimtembelea Sitta alipokuwa amelazwa katika hospitali moja jijini hapa.

Sitta ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba na waziri katika wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti, ni miongoni mwa wanachama zaidi ya 40 wa CCM waliochukua fomu za kugombea urais mwaka jana. Hata hivyo, baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kumuondoa, alitangaza kustaafu masuala ya siasa.


/ Mwananchi

TUJIKUMBUSHE KIDOGO MANENO YA SAMUEL SITTA JUU YA URAIA PACHA!!!
Akihojiwa na Voice of America Mh. Sitta amesema hawatatoa uraia pacha kwa sababu waZanzibar wa Oman watapindua nchi

No comments :

Post a Comment