dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 12, 2016

Maalim Seif amdhibiti Profesa Lipumba, benki kufungua akaunti!


Ashura Mustafa katika uhai wake akiamkiana na Maalim Seif Sharif Hamad (Katibu Mkuu wa CUF), kwa muonekano wa picha hii inaonekana imepigwa katika matukio ya karibuni sana. Picha kutoka kwenye mitandao ya kijamii

Na Mwandishi wa Mtanzania
Jumatano, Oktoba 12, 2016

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amemdhibiti mwenyekiti anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kwa kuziandika barua benki zote, ili kudhibiti ruzuku ya chama isipite kwenye mikono ya kiongozi huyo.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kumtambulisha Profesa Lipumba katika Benki ya NMB Tawi la Ilala, akitaka apewe ushirikiano wa kufungua akaunti mpya ya chama.

Taarifa kutoka ndani ya CUF zililiambia MTANZANIA kuwa juzi Maalim Seif, aliandika barua kwa benki zote kuzui hatua hiyo kwa kuweka zuio la mtu yeyote kufungua akaunti ya chama.

“Unajua hii vita si ya kitoto ni mapambano yaliyopo ndani ya CUF, lakini yana nguvu kubwa kutoka katika kila pembe ya watu wanaochukia upinzani. Na pia wapo hata viongozi wakubwa wa dola ambao kila siku wamekuwa wakifanya kazi ya kuivuruga CUF.”“Walitegemea lakini tangu jana (juzi) Katibu Mkuu ameziandikia barua benki zote nchini kuzuia mpango wa msajili kutaka kuchepusha ruzuku ya chama na kwenda katika mikono ya Lipumba na sasa nakala yake imepelekwa kwa Msajili wa Vyama,” alisema mtoa habari huyo.

Hatua ya Profesa Lipumba kufungua akaunti inatokana na barua aliyopewa na Msajili wa Vyama vya Siasa ya Oktoba 6, mwaka huu iliyosainiwa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza kwenda kwa Meneja wa Benki NMB Tawi la Ilala.

Katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba HA.322/362/14/104 ambayo inamtambulisha Profesa Lipumba kutakiwa kufungua akaunti mpya ya ‘The Civic United Front’ (CUF).

Kutokana na hali hiyo MTANZANIA (Gazeti la Mtanzania), lilimtafuta Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa Umma, Mbarara Maharagande ambaye alithibitisha kuandikwa kwa barua hiyo kwa benki zote nchini.

Siri ya Profesa Lipumba kutaka kufungua akaunti mpya yenye jina la Chama cha Wananchi CUF inadaiwa kutolewa na watumishi wa benki wa tawi hilo.

Profesa Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama.

Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kupitia Sisty Nyahoza, ilinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari ikikiri kumtambulisha Profesa Lipumba kwa Benki ya NMB, ili aweze kufungua akaunti hiyo. Huku, Ofisi ya Msajili ikikana kujua matumizi ya akaunti hiyo.

Taarifa za kufunguliwa kwa akaunti mpya yenye jina la CUF kwa malengo yanayodaiwa ni kuchukua ruzuku za chama hicho zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.

Hatua ya Profesa Lipumba ambaye kwa sasa yupo katika ziara kwenye mikoa ya kusini kutaka kufungua akaunti hiyo ilipingwa vikali na wana CUF akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya CUF (JUVCUF), Hamidu Bobali ambaye alitangaza kwa kuwataka wanachama wao kutompa ushirikiano kiongozi huyo katika ziara zake.

Profesa Lipumba ambaye ni mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama, amekuwa akifanya mikutano ya hadhara na ya ndani katika Mikoa ya Kusini, inayopewa ulinzi na Jeshi la Polisi.

Tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, Oktoba 25 mwaka jana, Jeshi la Polisi kufuatia kauli ya Dk John Magufuli limezuia shughuli za mikutano ya hadhara na maandano hasa kwa vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.

Maalim na Msajili tena
Katika hatua nyingine, Maalim Seif amemwandikia tena barua Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akimtaarifa kuhusu maamuzi ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi liloketi Septemba 27, mwaka huu.

Barua hiyo ya Oktoba 4 mwaka huu yenye kumbukumbu namba CUF/HQ/KM/2016/21, ambayo Maalim Seif amesema wamebaini kwamba pamoja na kuandikia mara kadhaa kwamba Ofsi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haina mamlaka, uwezo wala wajibu wa kuingilia maamuzi ya vikao halali vya chama.

“Pamoja na hali hiyo bado umekuwa ukituandikia na kututaka tujibu malalamiko ya watu waliowasilisha malalamiko kwako kuhusiana na maamuzi ya vikao halali vya chama.

“Uzoefu tulioupata kupitia barua yako Kumb. Nam. HA.322/362/14/85 ya tarehe 23 Septemba, 2016 iliyokuwa na kichwa cha maneno, “MSIMAMO NA USHAURI WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSU UONGOZI WA KITAIFA WA CHAMA CHA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF)”. inasema barua hiyo.

Wakati huo huo, Ashura Mustafa aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili, anaandika Faki Sosi wa mwanaHALISI online.

Ashura, aliyesimamishwa uanachama wa chama chake katika mgogoro wa ndani wa chama hicho unaoendela kwa sasa, hwenda maziko yake yakawakutanisha Maalim Seif Sharif Hamad na Profesa Ibrahim Lipumba.

Ashura, alikuwa amelazwa takriban kwa wiki moja kutokana na tatizo la upungufu wa damu mwilini na kwamba taratibu za maziko, zinafanywa na familia yake.

No comments :

Post a Comment