dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 30, 2016

BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YANGAMIZI ZAIDI YA TANI 62 ZA BIDHAA ZILIZOHARIBIKA!

  Wafanyakazi wa gari ya mizigo wakishusha bidhaa zilizoharibika katika dampo la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja tayari kwa kuangamizwa katika zoezi ililosimamiwa na Bodi ya Chakula, Dawa na vipodozi Zanzibar.
 Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) wakiwa katika maandalizi ya kuharibu chakula na dawa zilizoharibika na kupitwa na wakati katika dampo la Kibele.
 Magari ya mizigo yakishusha shehena za bidhaa mbovu zilizokamatwa na maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi katika maghala na maduka Zanzibar.
 Mkuu wa operesheni wa uangamizaji wa bidhaa mbovu wa ZFDB ndugu Abdulaziz Shaib Mohd akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuangamiza bidhaa hizo katika dampo la Kibele
Kijiko cha Manisapaa ya Zanzibar kikiharibu bidhaa mbovu na zilizomaliza muda wake wa matumizi katika dampo la Kibele Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar                   
Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imeangamiza zaidi ya tani 62 za vyakula vibovu na vilivyopitwa na wakati katika zoezi lililofanyika Kibele Mkoa Kusini Unguja.
Mkuu wa Idara ya Biashara na Uendeshaji wa ZFDB Ndugu Abdulaziz Shaib  Mohd amesema bidhaa hizo mbovu zinatokana na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kujenga matumaini ya kuingiza faida kwa  bidhaa wanazouza bila kuangalia usalama wa bidhaa hizo kwa afya za watumiaji.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamiza bidhaa hizo, Ndugu Abdulaziz ambae pia ni Mkuu wa operesheni wa uangamizaji amesema bidhaa hizo zimegundulika kufuatia operesheni iliyofanywa na Bodi katika maghala na maduka mbali mbali ya Unguja.
Amesema ZFDB ambayo moja ya jukumu lake ni kusimamia ubora na usalama wa chakula, dawa na vipodozi kwa matumizi ya wananchi, itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala yanayowekwa bidhaa na kwenye maduka ili kuhakikisha jukumu hilo linafanikiwa.
Amewataka wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa wananchi wenzao na kujuwa kwamba biashara mbovu ama zilizopitwa na wakati ni sumu na zinaweza kudhofisha afya zao.
Mkuu wa Idara ya Chakula wa ZFDB bibi Aisha Suleiman amesema  mchango mkubwa wa raia wema ndio uliofanikisha kugundulika  bidhaa mbovu na zilizopitwa na wakati katika maduka na maghala mbali mbali.
Hata hivyo amewataka wananchi kujenga tabia ya kuchunguza tarehe ya kumaliza muda bidhaa wanazonunua na wanapogundua bidhaa imepitwa na wakati watoe taarifa katika Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi  ili hatua  za haraka ziweze kuchukuliwa.
Wakati huo huo Afisa Mkuu wa Idara ya Dawa na Vipodozi wa ZFDB Ndugu Mwadini Ahmada Mwadini amesema vipodozi haramu vilivyokamatwa baadhi yake vinakemikali zenye sumu na hazifai kwa afya ya binadamu.
Amewashauri wafanyabiashara wanaotaka kuanzisha biashara ya dawa na vipodozi kushirikiana na Bodi hiyo kwa lengo la kulinda afya za wananchi.
Dawa zilizoangamizwa katika operesheni hiyo ni mafuta ya kula lita 10,105, sukari tani 2.15, mchele tani 26, tende tani 10, bidhaa  mchanganyiko za mboga mboga tani 13, dawa na vipodozi tania tatu.

No comments :

Post a Comment