Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Saturday, November 5, 2016

KILIO CHA WAKAAZI WA KWARARA!

  • Kwarara yaathirika!
  • Wakaazi wanalia kilio cha masikitiko!
  • Kwarara sio tena ile tunayoijua bali sasa ni shimo la mchanga la wenye tamaa!

Hawa wanaofanya uharibifu huu wanao uhakika kuwa hakiwezi kutokea kitu chochote dhidi yao na walifika hata kumcheka muandishi wetu wakati akichukua video hii hapa juu na huku wakitania kwa kuuliza picha zao watazipata saa ngapi?Inasikitisha na kuhuzunisha kuona kuwa eneo la Kwarara liliopo nje kidogo ya mji wa Zanzibar linaathirika vibaya sana, wakati wenye majukumu ya kuizuia hali hio mbaya wapo na wanajua kinachotokea, lakini wanayafumba macho yao kama vile waliolala usingizi wa maisha.

Muandishi wetu wa Zanzibar Ni Kwetu alifika leo asubuhi huko Kwarara kusikiliza kilio cha wakaaji wa eneo hilo na alichokiona kilishitua mpaka uti wake wa mgongo.

Muandishi alijionea mwenyewe vipi wachimba mchanga wanavyoliharibu eneo hilo lenye mandhari nzuri, ambalo huko nyuma wakaazi wa mjini Zanzibar walikuwa wakikimbilia kupunga upepo kwa kuliepuka joto la mjini.

Uharibifu huu sio wa mazingira tu bali mpaka mali za serikali, kama vile zile nguzo za umeme zinazoleta umeme Unguja kutoka DSM kupitia Fumba.

Nguzo za umeme zimo hatarini kutokana na wezi wa mchanga kuchimba katika kila eneo lenye mchanga.

Walivyoulizwa na muandishi wetu wenyeji wa Kwarara kwanini hawaripoti hali mbaya kama hii kwa vyombo vinavyohusika, mmoja alijibu kuwa wanaohusika wanajua kila kitu kinachoendelea, lakini hakuna anaejali.

"Tushapeleka habari kituo cha polisisi cha Fuoni na cha Meli Tano. Tushapeleka habari ZECO, tushapeleka habari Manispaa ya Mjini Magharibi (zamani ikiitwa Halmashauri), tushamjulisha Mbunge na Muakilishi wa eneo pamoja na jamaa wa Mazingira. Wote hao wamekaa kimya. Kubwa zaidi ni kuwa polisi wanatujibu kuwe eti tuwakamate hao wahalifu na tuwapeleke kituoni na hapo tena wao polisi ndio wataweza kuchukua hatua za kisheria". Alielezea mkaazi mmoja wa Kwarara huku akisikitika.


"Hii inamaana ukimuona mtu anafanya uharibifu wa mali ya serikali na ukawapigia simu polisi, basi ujue polisi hawatokuja isipokuwa watakueleza kuwa wewe umkamate huyo anaefanya uharibifu huo na uwapelekee wao kituoni, hapo tena ndio wao watachukua hatua za kisheria. Hivyo maneno haya yanaleta maana kweli jamani?", alimalizia mwananchi huyo.

Cha kusikitisha zaidi ni kuwa wananchi wa kawaida hawajui hasara ya mashimo haya ya mchanga na wengine wanajenga karibu nayo na kwavile ardhi yenyewe ni ya mchanga basi ikinyesha mvua kubwa nyumba zote hizi zitachukuliwa na maji (land sliding).

Muandishi anaeleza kuwa eneo lilioharibika sana ni Kwarara Kwa Ngurangwa, kwenye njia ya kuendea shule mpya ya serikali (Tumaini Secondary School) itakayofunguliwa karibuni kwenye sherehe za Mapinduzi. 

Maeneo ya ZECO yanayopita umeme wa kidato ndio yanayoshambuliwa zaidi na wachimba mchanga kwasababu maeneo haya hayana mmiliki wa kuyaangalia kila siku.
1 comment :

  1. Hii ni hatari.
    ZECO lindeni nguzo zenu za umeme!

    ReplyDelete