dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 20, 2016

Matayarisho ua Ufunguzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Yakamilika!

Mwonekano mpya wa Hospitali ya Abdalla Mzee, Mkoani ambayo inakaribia kumalizika ukarabati wake
Na Salmin Juma
Wananchi kisiwani Pemba, wametakiwa kuhudhuria kwa wingi katika ufunguzi wa hospitali mpya ya Abdalla Mzee Mkoani inayotarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 26 mwezi huu.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini pemba Mhe.Mwanajuma Majid Abdalla,wakati alipokuwa akizungumza na  maafisa wadhamini wa wizara zote za serikali na watendaji wa taasisi nyegine hapo katika hospitali ya Abdalla Mzee mkoani.

Amesma kuwa lengo la kuitisha mkutano huo nikuzungumzia  maandalizi ya ufunguzi wa hospitali hiyo unatarajiwa kufunyika wiki ijahyo ya mwezi huu  ambapo mgeni rasmi anatarajiwa katika ufunguzi huo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhamed Shein.Aidha amewataka maafisa wadhamini hao kuhakikisha kwamba kila alopangiwa dhamana ndani ya ofisi  yake ahakikishe anatekeleza wajibu wake.

Nae Mkuu wa Wilaya Mkoani Ndg  Hemed Suleiman Abdalla, ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajengea wananchi wake hospitali  ya rufaa kisiwani pemba hivyo hapana budi wananchi hao kuhudhuria kwa wingi siku ya ufunguzi kwani ni jambo la historia kubwa na la kujivunia kupata kitu hicho kwao.

Hata hivyo amemuoba afisa mdhami wa shirika la umeme pemba kuhakikisha kipindi hiki cha matayarisho ya ufunguzi wa hospitali umeme uwepo muda wote pamoja na kuongeza bidii za kukamilisha ukarabati wao ili kuweza kupata umeme wa uhakika .

Kwa upande wake mkurugenzi wa wizara afya Zanzibar Mohd Dahoma amesema kwamba maandalizi yako hatua mzuri hivyo amewahimiza wananchi kuungana nao ili kuona wanasherehekea ufunguzi huo wa hospitali hiyo mpya ya kisasa.

No comments :

Post a Comment