Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Thursday, November 24, 2016

WADHAMINI WA CUF WAMKATAA JAJI KIHIYO NA KUMTAKA AJITOE!

Image result for CUF FLAG

THE CIVIC UNITED FRONT

(CUF–Chama Cha Wananchi)
DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION

P.O.BOX 10979 DAR ES SALAAM
Director: Salim Biman Zantel No. 0777 414 112 / Voda No. 0752 325 227
A/Deputy Director: Mbarala Maharagande Airtel No. 0784 001 408 / Halotel No. 0621 715 795

TAARIFA KWA UMMA
Imetolewa leo Tarehe 24/11/2016
Na Mbarala Maharagande- K/Naibu Mkurugenzi Habari.
WADHAMINI WA CUF WAMKATAA JAJI KIHIYO NA KUMTAKA AJITOE KUSIKILIZA SHAURI HILI LA MADAI NAMBA 23/2016. SHAURI LIMEAHIRISHWA NA KUPANGWA KUSIKILIZWA
TAREHE 6 DECEMBER, 2016
LEO Tarehe 24/11/2016 Mbele ya Jaji Kihiyo Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, mawakili wasomi Juma Nassor na Hashimu Mzirai wamewasilisha ombi la kumtaka Jaji Kihiyo Kujitoa kusikiliza shauri hili kutokana na wateja wao (THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) sababu za msingi zilizotolewa zitaelezwa tarehe 6/12/2016 kutokana na Jaji kihiyo kudai kuwa bado hajapokea Barua hiyo ambayo imefailiwa mahakamani hapo jana tarehe 23/11/2016. Baada ya majibizano makali ya kisheria na kuwepo kwa mapingamizi kwa pande zote mbili dhidi ya mwingine (Upande wa Lipumba na wenzake umeweka pingamizi juu ya hati ya kiapo (Affidavit) na upande wa CUF imeweka pingamizi juu ya majibu ya hati ya kiapo (Counter Affidavit) iliyowasilishwa kutoka upande wa Lipumba na wenzake) aidha pande zote zilikamilisha kuwasilisha nyaraka zake kwa wakati ambapo upande wa Lipumba na wenzake uliwasilisha tarehe 17/11/2016 na upande wa CUF ulifaili majibu yake tarehe 23/11/2016 kama ilivyopangwa awali tarehe 10/11/2016.
Kutokana na Hoja hizo na Jaji Kihiyo kuomba kwamba tukamilishe hatua hii ya awali (proceed) tarehe 6/11/2016 saa 7:30 Mchana litawasilishwa rasmi ombi la kumtaka ajitoe na kuelezwa sababu zake na hapo ndipo kwa upande wake atapanga kulitolea maamuzi ombi hilo kwa kukubali kujitoa au kukataa.
VURUGU MAHAKAMANI:
Walinzi wa Lipumba walianzisha vurugu zisizo za lazima kwa kutaka kuwazuia viongozi wa CUF akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ABDALLAH KHATAU wasiweze kuingia katika Chumba cha Jaji kusikiliza shauri lao hata hivyo walinzi wa chama waliweza kuwadhibiti na kuhakikisha viongozi hao wanaingia ndani jambo ambalo halikuwa na mantiki yoyote. Walinzi wa Lipumba sio watendaji wa Mahakama kwa hiyo hawana mamlaka ya kufanya walivyotaka kufanya. Wakati haya yakitokea ndani ya ‘corridor’ za mahakama kuu huko nje mapambano yaliendelea na kupelekea Jeshi la Polisi kuingilia kati hata hivyo hakuna aliyedhurika. Ni vyema vyombo vya ulinzi vikatekeleza wajibu wake na kwa upande wetu hatutakubaliana na upuuzi wowote utakaofanywa na wahuni hao dhidi ya wanachama na viongozi wa CUF. Kutokana na wingi wa watu na kuepusha vurugu hizi Jaji Kihiyo ameshauri wakati ujao itumike mahakama ya wazi (Open-Court) ili kutoa fursa kwa washiriki wengi zaidi kuweza kufuatilia na kujua kinachoendelea.
MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI:
Baada ya shauri kuahirishwa Lipumba na wenzake walichukuliwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi wakitokea mlango unaotumiwa na Majaji kutoka nje kuepusha kukumbana na wanachama waliokuwa na hasira kali dhidi ya haya yanayoendelea. Viongozi wa Taasisi ya CUF-Chama Cha Wananchi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya CUF Abdallah khatau, Naibu katibu mkuu na mkurugenzi wa uchumi na fedha Joram Bashange, Naibu Mkurugenzi wa Oganazizesheni na Uchaguzi- Mhe. Shaweji Mketo, kiongozi wa wabunge wa CUF Bungeni Bi Riziki Shaali, Muandishi wa taarifa hii na viongozi na wanachama wengine wengi waliohudhuria mahakamani hapo walipata fursa ya kufanya mahojiano na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mahakamani hapo kujua nini kinaendelea baada ya kutoka mahakama hapo.
Shauri hili lililofunguliwa tarehe 19/10/2016 na THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) dhidi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini (THE REGISTRAR OF THE POLITICAL PARTIES)-1, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (THE HONOURABLE ATTORNEY GENERAL)-2, Prof Ibrahim Haruna Lipumba-3, Magdalena Sakaya-4, Maftaha Nachuma-5, Abdul Kambaya-6, Masudi Omari Mhina-7, Thomas Malima-8, Kapasha H. Kapasha-9, Musa Haji Kombo-10, Habibu Mnyaa-11, Na Haroub Shamis-12.
Katika shauri hili la madai THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) inaiomba mahakama itoe amri ya kubatilisha barua ya Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi inayotoa maoni, ushauri na msimamo wa ofisi yake kuitaka CUF imtambue Lipumba kuwa Ni ‘Mwenyekiti wake Halali’, pia CUF inaiomba mahakama kuu itoe amri ya kumzuia Msajili wa vyama vya siasa nchini kufanya kazi nje ya mipaka yake ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yake na itoe amri ya kumzuia Msajili wa vyama vya siasa nchini kuacha mara moja kuingilia masuala ya kiutawala na kiutendaji ya shughuli za ndani ya chama chetu cha CUF. Na msingi wa maombi haya yamebainishwa katika hati ya Kiapo kinachounga mkono maombi hayo na kusainiwa na Maalim Seif Sharif Hamad kwa niaba ya wadhamini wa CUF kinasisitiza na kubainisha wazi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kuingilia utendaji wa ndani wa Vyama vya Siasa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Katiba ya nchi ambayo haimpi mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuwa chombo cha rufaa wala kurejea na kufanyia maamuzi mambo ya utawala ndani ya chama cha siasa. Mamlaka hayo yapo kwa vyombo vya juu vya chama kwa mujibu wa katiba ya CUF na au Mahakama pekee.
Majukumu ya Msajili yameainishwa katika sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2008 (The political parties Act, 2008) miongoni mwayo ni kusajili vyama, kupokea na kuhifadhi kumbukumbu za vyama hivyo ikiwemo taarifa za fedha, orodha ya viongozi wa kitaifa, anuwani za vyama na mahala ofisi za vyama hivyo zilipo nakadhalika.
THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) inawakilishwa na Mawakili wasomi Mhe. Daimu Halfani, Mhe. Juma Nassor, Mhe. Hashimu Mzirai, na Mhe Twaha Taslima. wakati Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi na Mwanasheria Mkuu wa serikali wanawakilishwa na Wakili wa serikali (PSA), Gabriel Malata badala ya Obadia kameya ambaye alikuwepo tarehe 10/11/2016. Aidha, Lipumba na wenzake wamewakilishwa Mashaka Ngole ambapo Albert Msando ambaye ni wakili wa kujitegemea anayetoka chama cha ACT-Wazalendo hakufika mahakamani na hakuna sababu zilizotolewa za kutofika kwake. Wadaiwa wote walihudhuria mahakamani isipokuwa wadaiwa namba 6, 9, na 10 katika orodha tajwa hapo juu. Mawakili wetu wametuhakikishia kuwa wamejipanga vizuri na kuwataka wanachama na wapenzi wote wa CUF kuendelea kuwa watulivu na wenye subra wakati wakiendelea kuandaa mikakati mbalimbali ya kujenga HOJA dhidi ya wadaiwa wote katika shauri hili. Tunawapongeza wanachama wetu wote na walinzi wa chama NGANGARI (Blue Guard) kwa kujitokeza kwa wingi na kuwalinda vyema viongozi wetu wote dhidi ya wahuni wachache waliokusudia kutaka kuanzisha fujo mahakamani. Tunawaomba tukutane tena kwa wingi mahakamani tarehe 06 DECEMBER, 2016 saa 7:30 Mchana katika mahakama ya wazi ili kila mmoja wetu apate nafasi ya kusikiliza na kushuhudia hoja makini kabisa na mawakili wetu wasomi.
WENZETU WACHANGANYIKIWA:
Baada ya kuwasilishwa hoja za kumtaka Jaji Kihiyo kutakiwa kujitoa kusikiliza shauri hili ambayo ni matakwa ya kisheria na kusudio la kuweka pingamizi dhidi ya hati ya majibu ya kiapo (Counter Affidavit) zao wamechanganyikiwa na wametoka vichwa chini hatutujui wametokomea wapi kujipanga upya. HAKIKA HAKI ITAPATIKANA.
Chama cha CUF kinaamini kuwa; “utawala wa sheria na mahakama huru ndio ngao kubwa ya demokrasia ya nchi yetu” (katiba ya CUF ibara 6(5) katika ibara ya 7(5) inayozungumzia Lengo na madhumuni ya chama inaeleza wazi kuwa“ kuondoa mambo yote yanayoruhusu rushwa, ufisadi, ubadhilifu, uonevu, ukandamizaji na ubaguzi wa aina yeyote” haya ni katika madhumuni ya chama cha CUF.

CUF NI TAASISI IMARA, HAKI SAWA KWA WOTE

____________________________________
MBARALA MAHARAGANDE
K/NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA

MAWASILIANO: Airtel-0784 001 408 Vodacom: 0767 062 577 Tigo: 0715 062 577 email:maharagande@gmail.com

No comments :

Post a Comment