Taarifa ambazo Nipashe ilithibitishiwa na kiwanda cha Dangote jana, zilieleza kuwa Dangote anakuja nchini kwa nia ya kumuona Rais Magufuli ili ashitakie mambo kadhaa ikiwamo madai ya kuwapo kwa hujuma anazofanyiwa na baadhi ya watu kwa sababu za kibiashara.
Kiwanda cha Dangote ambacho ni kikubwa zaidi Afrika Mashariki kwa uzalishaji wa saruji, kilisitisha uzalishaji wiki mbili zilizopita kutokana na kile kilichoelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Harpreet Duggal, kuwa ni kuelemewa na gharama kubwa za uendeshaji.
Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti, aliiambia Nipashe jijini Dar es Salaam jana jioni kuwa 'bosi' wake ameamua kuja nchini kuzungumza na Rais Magufuli juu ya vikwazo vinavyoukabili mradi huo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 500.
"Kuna mambo mengi tuliyokubaliana na Serikali kabla ya kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na hatuna tatizo na serikali. Imetupa msamaha wa kodi kwenye mambo mengi kuanzia ardhi, mafuta ya dizeli lita milioni tatu na mengine mengi," alisema Baruti.
http://www.jamiiforums.com/threads/dangote-ajiandaa-kuongea-na-rais-magufuli.1161501/
No comments :
Post a Comment