Meli ya Titanic iliyojengwa na Harland na Wolff huko Belfast, iligonga mwamba wa barafu na kuzama Kaskazini mwa Atlantic mwaka 1912 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,500 ilikuwa katika safari yake kutoka Southampton ikielekea New York.
Leo ikiwa ni takribani miaka mia na nne ‘104’ imepita tangu meli hiyo izame, China wameamua kujenga meli inayofanana na Titanic, habari kuhusu meli hiyo imewashangaza raia wengi wa China baada ya ujenzi huo wa meli hiyo yenye urefu wa kina cha mita 269 kuanza.Meli hiyo ya China, itakuwa yenye umbo sawa na ile ya Titanic, itakuwa na sehemu ya michezo, maonyesho, kuogelea na sehemu maalum ya watu maalum ambayo itakuwa na mtandao wa Wifi na inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika eneo hilo la theme park lililoko kilomita kadhaa kutoka pwani ya China.
Meli ya Titanic mwaka 1912 ilipokuwa ikifanya ikitoka Southampton ikielekea NewYork
Ujenzi huo wa meli hiyo yenye urefu wa kina cha mita 269, itawekwa katika hifadhi iliyoko mashambani, katika mkoa wa Sichuan
Chakula kitakachotolewa kwenye meli hakitatofautiana na kile ambacho kilitolewa Meli ya Titanic 1912
Chumba cha gharama zaidi kitakuwa ni Yuan 100,000 , sawa takribani Tsh 31,521,912
/Muungwana
No comments :
Post a Comment