Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 5, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI WA MAUZO WA KAMPUNI YA NDEGE YA BOEING, MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) PAMOJA NA BALOZI WA CUBA HAPA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo pamoja na ujumbe wake.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama kitabu cha  picha ya ndege aina ya Boeing 787-8 Dream liner wakati alipokuwa akisikiliza maelezo yake kutoka kwa Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo. Ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 262 na itakuwa na uwezo wa kuruka kutoka nchini Marekani hadi Tanzania bila kutua mahali popote.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mkurugenzi wa mauzo wa Kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Doto James na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kuhusiana na ununuzi wa ndege hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dream liner mara baada ya kumaliza mazungumzo na Mkurugenzi wa mauzo wa Kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake nchini George Luis Lopez Tormo aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake hapa nchini George Luis Lopez Tormo aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuaga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake hapa nchini George Luis Lopez Tormo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Dkt. Tonia ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo Afrika ya Kusini
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero ambaye alifika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na kuagana na Mhe. Rais Dkt. Magufuli. Dkt. Tonia ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo Afrika ya Kusini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero ambaye alifika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.Dkt. Tonia Kandiero ameteuliwakuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo Afrika ya Kusini.
 PICHA NA IKULU 

No comments :

Post a Comment