dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 10, 2016

SHIRIKA LA NDEGE LA UTURUKI LAANZISHA SAFARI ZAKE ZANZIBAR!

Tanzania inakuwa nchi ya 50 barani  Afrika kufikiwa na Shirika la Ndege la Uturuki baada ya kuongezwa safari tatu kwa wiki kwenda Zanzibar

Shirika la Ndege la Uturuki limeiongeza Zanzibar katika mtandao wa safari zake kuanzia Desemba 13, 2016. Hivi sasa shirika hilo linafanya safari 49 barani Afrika baada ya hivi karibuni kuongeza safari ya kwenda Visiwa vya Shelisheli.

Shirika hilo maarufu barani Ulaya kwa sasa linafanya jumla ya safari 293 duniani kote, zikiwemo safari 50 kwenye nchi 31 za Afrika.

Likiwa ni shirika la nne kwa kuwa na mtandao mkubwa wa safari duniani kote kuliko mashirika mengine, Shirika la Ndege la Uturuki sasa litahudumia miji ya kimataifa 244 ikijumlishwa na Visiwa vya Zanzibar ambavyo ni maarufu kwa biashara ya viungo.
Watumiaji wa ndege za shirika hilo sasa watafurahia uzoefu watakaoupata kutokana na safari hizo mpya zinazojumuisha miji 20 maarufu duniani kama vile Frankfurt, Muscat, Munchen, Dubai, Paris, London, Milano, Amsterdam, Zurich, Bombay, Copenhagen, Stockholm, Rome, Brussels, Berlin, Vienna, Hamburg, Tel-Aviv, Düsseldorf, na Prague.

Safari ya kwanza itazinduliwa Jumanne, Desemba 13, 2016 na wasafiri wataondoka Istanbul saa 6:30 usiku na ndege TK567 itakayowasili saa 3:30 asubuhi. Watarudi na ndege hiyo TK567 itakayoondoka Zanzibar saa 4:25 asubuhi na kuwasili Istanbul saa 11:45 jioni.

Safari za Instanbul – Kilimanjaro – Zanzibar – Istanbul (IST-JRO-ZNZ-IST)zitakuwa tatu kwa wiki. Utaratibu wa kuweka mpango wa safari unapatikana kupitia tovuti www.turkishairlines.com kama ifuatavyo:

Taarifa zaidi kuhusu ratiba ya safari:
Namba ya ndege 
Kuanzia
Siku
Kuondoka
Kuwasili
TK 567
14 Desemba 2016
Jumatatu Jumatano Jumamosi
Istanbul
20:30

3:20         (+1)
Kilimanjaro
TK567
15 Desemba 2016
Jumanne Alhamis Jumapili
Kilimanjaro
04:15
5:30
Zanzibar
TK 567
15 Desemba 2016
Jumanne, Alhamis Jumapili
Zanzibar
06:25
13:45
Istanbul


No comments :

Post a Comment