Na Salmin Juma Pemba
MKUU wa Wilaya Chake Chake Mhe: Salama Mbarouk Khatib amewataka vijana kuyatumia mabaraza ya vijana kwa kuhakikisha wanafanya shughuli walizojipangia , ili kujikomboa na umasikini na kuweza kujiletea maendeleo kiuchumi.
Akizungumza katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Chake Chake katika uwanja wa Tenis amesema, lengo la kuwekwa mabaraza ya vijana ni kuwa, mategemeo makubwa ni kuleta chachu ya maendeleo katika jamii.
Mkuu huyo amesema kuwa, kila kijana anatakiwa atimize wajibu wake, hivyo ni vyema wakafuata muongozo wa mabaraza, ili kuweza kuleta mabadiliko mbali mbali kiuchumi, kijamii, kisiasa na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Khadija Khamis Rajab amewataka vijana hao kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita suala la udhalilishaji katika jamii na kuweza kuviripoti vitendo hivyo kwa haraka pindi vinapojitokeza.

Akisoma risala Mjumbe wa baraza hilo Ibrahim Salum Rashid amesema, kuna changamoto nyingi zinazowakabili, ikiwa ni pamoja na kukosa ofisi maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji, ambazo zinawasaidia kujikwamua na umasikini.
Hata hivyo mwenyekiti wa Baraza hilo, Bakar Hamad Bakar amewataka vijana hao kufanya kazi kwa bidii zitakazowaletea mapato yatakaweza kuwakwamu hali ngumu ya maisha.
No comments :
Post a Comment