Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kwa mara nyingine wametwangana tena makonde mahakamani.
Leo ni mara ya pili kwa wafuasi na wanachama wa chama hicho kutwangana makonde mahakamani wanapofika kusikiliza kesi inayozihusisha pande mbili za chama hicho. Pande hizo ni kati ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad. Ugomvi huo ambao umewahusisha walinzi wa viongozi wa chama hicho maarufu kama mabaunsa wa pande hizo mbili umezimwa na askari polisi. Kwa sasa wafuasi wa pande zote wameingia mahakamani wanasubiri jaji aingie kwa ajili ya kusoma ya kusoma uamuzi wa maombi ya upande wa Maalim Seif kumtaka Jaji Sekieti Kihiyo anayesikiliza kesi hiyo ajiondoe kwa madai kuwa hawana imani naye. |
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Wednesday, December 14, 2016
WAFUASI WA CUF WATWANGANA TENA MAHAKAMANI!
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

No comments :
Post a Comment