Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Uzinduzi wa Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi uliofanyika tarehe 1 Desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe katika vitendea kazi kama ishara ya Uzinduzi wa Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi uliofanyika tarehe 1 Desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha vitendea kazi atakavyovikabidhi kwa bodi mara baadaya ya kuizindua Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi uliofanyika tarehe 1 Desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi Bw. Godfrey Simbeye vitendea kazi vya bodi hiyo mpya katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika tarehe 1 desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua Bodi ya Udhamini dhidi ya UKIMWI na kuwagawia vitendea kazi sambamba na uzinduzi wa mpango wa hiari wa familia kuchangia mfuko wa UKIMWI, shughuli iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo huadhimishwa duniani kote desemba mosi.Madhumuni ya Bodi hiyo ni kujenga nguvu ya ndani ya kifedha pamoja na kuhakikisha uwepo wa rasilimali za kutosha katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi ambao bado ni tishio huku tafiti za mwaka 2015 zikionesha kuwa takribani watu 48,000 huambukizwa VVU kila mwaka nchini, huku watu milioni 1.5 wakiishi na VVU kati yao wastani wa laki nane wanatumia dawa za kufubaza virusi vinavyosababisha UKIMWI.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais amesema kazi kubwa ya kutafuta kutunisha mfuko itakuwa ni chachu katika kupambana na ugonjwa huo na kuitaka bodi hiyo kubuni mbinu za kutunisha mfuko huo kufuatia ukweli kwamba uhisani una mwisho na uhisani una vipaumbele vyake kutokana na wakati husika.
Katika harambee iliyofanyika jana usiku wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo,zaidi ya milioni 340 zilipatikana.
No comments :
Post a Comment