Barua ya wazi kwa IGP wa Polisi
Mkuu wa Polisi Tanzania,
IGP,
Dar es salaam.
Niruhusu nikuandikie barua hii ya wazi kwa sababu napenda wananchi wenzangu wajue nilichokuandikia kwa vile matukio ya Jeshi letu la Polisi dhidi ya raia yanatuhusu sote, hata wewe mwenyewe kesho na keshokutwa ukirudi uraiani.
Sikuandikii kwa kuwa mimi hodari au jabari, la hasha, mimi ni mnyonge na mtu mdogo sana, lakini naona ni haki yangu ya kiraia kulisema jambo hili, japo pengine nitafikwa na madhara kwa ukweli wangu huu.

Ndugu IGP niruhusu nianze kwa mkasa mmoja ambao ulitokea huko Pemba baada ya raia mmoja kukamatwa na kupelekwa kituoni ambako inaelezwa kuwa Mkuu wa Kituo aliamuru mtu huyu apewe chai na askari mmoja akamtandika kibao kizuri.
Mtu huyo alifikiri vizuri na baada ya kuona hakuna sababu ya kuonewa naye alimtandika kibao kizuri askari aliyempiga na hata kubidi Mkuu wa Kituo kuhoji kwa nini ameipiga “dola” kama ambavyo tumesikia wenzetu wakijiita.

Bila ya kutafuna maneno raia aliyepigwa alisema, “Amenipa chain na mimi nikaona wajibu wa kumrudishia kikombe chake.”
Mkasa mwengine Ndugu IGP ni uliomtokea mwanangu wiki iliyomalizika pale alipokamatwa na kulazwa selo siku mbili kwa sababu aliwaambia askari waliokuwa wamemkamata raia kuwa wamtendee haki mtu waliyemkamata kwa kuwa alikuwa amejeruhiwa, akaambiwa anaingilia kazi za askari na amezuia askari wasifanye kazi zao.
Mkasa wa tatu ni wa kijana mmoja ambaye kwa wiki nne sasa yupo katika Kituo cha Polisi cha Makadara akisota bila kupelekwa Mahakamani kwa sababu alikamatwa kwa kosa la kuzurura, ilhali inajulikana kabisa mamlaka ya Polisi kumuweka raia kituoni ni kwa muda maalum. Yupo hana la kufanya na hana wa kumsaidia.Mkasa mwengine Ndugu IGP ni uliomtokea mwanangu wiki iliyomalizika pale alipokamatwa na kulazwa selo siku mbili kwa sababu aliwaambia askari waliokuwa wamemkamata raia kuwa wamtendee haki mtu waliyemkamata kwa kuwa alikuwa amejeruhiwa, akaambiwa anaingilia kazi za askari na amezuia askari wasifanye kazi zao.
Na tukio la mwisho ili nijielekeze katika barua yangu ni picha ambayo nimeiona katika gazeti la wiki iliyomalizika wa askari wetu wa kike akimuelekeza bunduki ya kifua Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Professa Ibrahim Lipumba baada ya kukamatwa kwa madai ya kuandamana bila kibali. Picha ile imenishitua sana na nimekuwa nikijiuliza masuali mengi.
Ndugu IGP hiyo ndio taswira ambayo ni uhalisi wa Jeshi letu la Polisi kwa wakati huu. Sijui mwenzetu ukiwa ndani unaiona au angalau wadogo wako wanafika kukuambia au umebanwa kama katika ile kadhia ya Mfalme aliyekuwa akienda uchi, lakini hakuna aliyeweza kumwambia, na makengele yake yakawa yanagonga huku na huku?

Sina hakika iwapo IGP unatizama video za matukio ambayo Polisi wetu huwa wanahusishwa na kulaumiwa kuwa wanakuwa katili kupita kiasi na kupita taratibu ambazo wenzetu hupenda kuziita zinazofaa kwa wakati ( reasonable force) ambapo huwa tando kwa nchi na sio kwa kisigino tu.
Sijui IGP huwa unajisikiaji kama askari uliyefunzwa ( professional policeman) unapoona askari wetu wanapompiga mwanamke mateke na virungu kwa sababu tu ameandamana, au mtu ambaye yupo chini na hana dhamira yoyote ya kukataa kukamatwa wala kumpiga Polisi akitandikwa virungu na kundi la askari wetu bila huruma na wala bila kinga?
Halafu niulize kwani wewe IGP si binaadamu kama sisi raia wengine, na kama ni hivyo unajisikiaje jioni ukiwa kwako unapotizama televisheni au unapokuwa ukisoma magazeti ni kuona vitendo vinavyofanywa na askari wetu? Au zama hizi za mtandao unaopoona Jeshi unaloliongoza linafanya vitendo vya kukiuka haki na maadili?

Hivi huwa unampimaje askari wako huyo anayefanya hivyo? Amefanya au anafanya wajibu wake? Amekiuka mipaka yake ya uaskari? Kama amefanya wajibu wake kumbe wajibu wake ndio huo tuelewe? Na kama amekiuka mipaka yake ya uaskari hatua gani zinachukuliwa? Na kweli hatua zinachukuliwa hata matukio tunayoyaana wazi wazi katika zama hizi za utandawazi?
Huwa tunajiuliza hivi hawa askari wetu wakifanya vitendo vya Nuni na Firauni wanaporudi vituoni hali huwa ipi?
Huwa tunajiuliza hivi hawa askari wetu wakifanya vitendo vya Nuni na Firauni wanaporudi vituoni hali huwa ipi?
Hupongezwa au hupongezana? Hujisifu au kusifiana? Wallahi sipati picha kabisa maana waliowapiga kupita kiasi, au waliowamwagia washawasha kupita kiasi ni raia wenzao, na hujiuliza mara zote hatua zote za kutuliza au kudhibiti zilitimizwa?
Pia hujiuliza sisi tuna vigezo tofauti na wenzetu duniani? Hivi Polisi wa nyengine wakiuka mipaka hufanywa nini? Jee wale wanaonekana wazi wazi wakipiga, kujeruhi huwa wanafanywa nini ndani ya Jeshi? Jee raia hawapaswi kujua hatua zinazochukuliwa? Na jee raia wanayo haki ya kupiga kulele? Ni wajibu gani wa Polisi kusikiliza makelele ya wananchi na kuyafanyia kazi?

Hivi kujikinga kwa hoja za kujitetea na kama vile kilichofanywa hakina neno Ndugu IGP huoni kuna hasara zaidi kwa sura ya Jeshi na uhusiano na raia ambao ndio lengo kuu kuwalinda wao na mali zao? Hivi haitafika siku, ambayo pengine haiko, mbali kutakuwa hakuna tena sababu ya kusema kwa matendo yanayofanywa?
Kule juu nilipoanza nilikuwekea Ndugu IGP matukio manne ili makusudi uone namna ambavyo sisi wananchi tunalitizama Jeshi letu. Tunapenda liwe Jeshi letu lakini linatukimbia. Tunapenda liwe ndio kimbilio letu lakini tunaliogopa. Tunapenda liwe kinga yetu lakini linatutisha. Tunapenda liwe ndio salama yetu lakini ndio nakama yetu.
Kila raia hupenda kutekeleza sheria bila kushurutishwa, lakini kila Polisi nae ana wajibu wa kutengeza mazingira ambapo raia analiamini Jeshi la Polisi, lakini Ndugu IGP una kazi kubwa ya kufanya na mimi siwezi wala sipendi kukufundisha kazi, ila najua una kazi kubwa.
Najua kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kusimamiwa na Sheria ya Kikoloni, lakini si tumekuwa huru kwa miaka 50 na zaidi hivi sasa? Raia wanajua na wanadai zaidi haki zao hivi sasa na ni lazima Polisi nayo iishi katika muktadha huo.
La sivyo Ndugu IGP naogopa isifike siku raia anaepewa chai na Polisi akaona ni haki yake na yeye kurudisha kikombe. Maana hivyo ndivyo itavyokuwa pale Polisi hawatotenda na kulinda haki na haki hiyo kuonekana ikitendwa, Nchi haiwezi kwenda kama haina Haki za Binaadamu.
Nashukuru kwa kuisoma barua yangu na inshallah umewaidhika, ila huna lazima ya kunisikiliza kwa kuwa wewe bado ni IGP wetu fanya kazi yako tu, lakini sote mwisho tutarudi kwa Mungu na Polisi wote watahukumiwa kama binaadamu wengine.
FB

No comments :
Post a Comment