Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 4, 2017

Rais Dk Shein afanya uteuzi wa Katibu Mkuu na manaibu Katibu!

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. AliMohamed Shein, anaonekana akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Nd. Yakout Hassan Yakout, katika wadhifa wake huo uliyopita. Hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika Ikulu Zanzibar. Bwana Yakout sasa amepata wadhifa mwengine na ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, jana tarehe 3 Febuari, 2017 amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za Serikali kama ifuatavyo:

1. KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA:


Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (2) na (3) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais amemteua Bibi Asha Ali Abdulla kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.
Aidha kwa mujibu wa kifungu cha 12 (3) cha sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011, Rais Dk. Shein ametengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Juma Malik Akili na atapangiwa kazi nyengine.

2. KATIBU MKUU WA OFISI YA RAIS, KATIBA, SHERIA , UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA:


Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (2) na (3) cha katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais amemteua Bwana Yakout Hassan Yakout kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

3. NAIBU KATIBU MKUU WA OFISI YA RAIS, KATIBA, SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA ANAYESHUGHULIKIA UTUMISHI WA UMMA:

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (4) cha katiba ya Zanzibar ya 1984, Mhe. Rais amemteua Bwana Seif Shaaban Mwinyi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora anayeshughulikia Utumishi wa Umma.

Uteuzi huo umeanza tarehe 3, Febuari, 2017.

No comments :

Post a Comment