Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 23, 2017

Gwajima: Mimi ndicho chanzo cha Nape kuondolewa uwaziri!

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima amesema kuwa yeye ni sababu kubwa ya  kutenguliwa kwa Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye. 
By Cledo Michael,Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz.
Dar esSalaam.Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima amesema kuwa yeye ni sababu kubwa ya  kutenguliwa kwa Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye.
Akizungumza leo (Alhamisi) baada ya kutembelea Ofisi za kituo cha redio cha Efm,Gwajima amesema    Mkuu wa Mkoa alivamia  ofisi za  Clouds kwa lengo la kutaka wamchafue Askofu huyo lakini baada ya Nape kuunda tume iliyofanya uchunguzi kumesababisha kutenguliwa kwake.
"Labda niseme kuwa sababu za Nape kutenguliwa zinanihusu sana mimi.Cha kujiuliza ni kwamba ni nani alikuwa nyuma ya Mkuu wa Mkoa alipovamia Clouds hadi Nape atenguliwe?”alihoji.
Gwajima alifika Ofisini hapo saa 4:06 na kukutana na viongozi na wafanyakazi huku akiwapa pole na kuwatia moyo na kwamba watayashinda majaribu yanayoikumba tasnia ya habari.

No comments :

Post a Comment